Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Mhe. Maabad Suleiman Hoja amekabidhi hundi za mikopo isiyo na riba kwa vikundi 49 vya vijana wajasiliamali kutoka katika kata za Mji mwema, Kibada, Kimbiji, Tungi na Somangila yenye thamani ya Milioni 113.
Mhe. Maabad Suleiman Hoja amewasisitiza vijana kutumia mikopo hiyo kama chachu ya kuleta maendeleo katika jamii zao na kuwaongezea kipato kwa kuzingatia kuwa tayari vijana hao wameshapatiwa mafunzo elekezi ya masomo ya biashara, utunzaji wa kumbukumbu za fedha, pamoja na utaratibu mzima wa urejeshaji wa mikopo hiyo.
Akisoma taarifa ya utoaji hundi za mikopo hiyo, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Ndg. Bakari Said Mnkeny amesema kuwa kabla ya vikundi vya vijana kupatiwa mikopo isiyo na riba taratibu zinazotakiwa kufanyika ni pamoja na usajili wa vikundi, uhakiki wa kikundi chenyewe kama kiko hai na usahihi wa taarifa zilizowasilishwa na kikundi ambapo taratibu hizo zimefuatwa katika kuvipata vikundi hivyo.
Aidha Ndugu Mnkeny ameongeza kuwa kwasasa Halmashauri imetoa Mkopo wa Milioni 113 kwa awamu ya kwanza kwa jumla ya vikundi 49 ambavyo vimekidhi vigezo vya kupatiwa mkopo huo na orodha ya vikundi vingine 33 inaendelea kuandaliwa kwaajili ya kupatiwa mikopo katika awamu ijayo.
Mwisho Mstahiki Meya amewasisitiza vijana kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kuwezesha vikundi vingine kuweza kunufaika na mikopo hiyo katika awamu zijazo.
Pichani ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Mhe. Maabad Suleiman Hoja akikabidhi hundi za mikopokwa wawakilishi wa vikundi vya vijana wajasilimali
|
Pichani ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Mhe. Maabad Suleiman Hoja akikabidhi hundi za mikopo kwa wawakilishi wa vikundi vya vijana wajasilimali
|
Pichani ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Mhe. Maabad Suleiman Hoja akikabidhi hundi za mikopo kwa wawakilishi wa vikundi vya vijana wajasilimali
|
|
Maafisa maendeleo ya jamii wakitoa maelekezo kwa viongozi wa kila kikundi mara baada ya kupokea hundi
|
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa