Mbunge wa Kigamboni na Naibu waziri wa Afya Wazee Jinsia na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile jana amekabidhi ambulance (gari ya kubebea wagonjwa) kwenye hospitali ya Vijibweni kwa kushirikiana na Ubalozi wa Australia nchini Tanzania (Autsralia Tanzania society) kwa lengo la kutoa huduma nzuri kwa wananchi wa Kigamboni .
Wakikabidhi gari hilo Dkt.Faustine alisema kuwa anaomba gari hilo litumike kwa malengo yaliyokusudiwa kwani hatarajii kukuta au kuelezwa kuwa linafanya kazi kinyume na taratibu kwasababu lengo lake ni kuhakikisha sekta ya afya inasimamiwa imara na ikiwezekana Kigamboni iwe ya Mfano
“Kigamboni ni Wilaya Mpya ila inapiga hatua kwa haraka sana,Napenda mtu akija kigamboni kwenye suala la afya aone kweli huu ni mfano ambao unaweza kuigwa sehemu nyingine yoyote , tusijekukuta gari hizi zinabeba mikaa huko” alisema Dkt.Faustine
Aidha Mbunge alitoa rai kwa watumishi wa afya wa Manispaa ya Kigamboni kuendelea kutoa huduma kwa upendo , kuhakikisha dawa zinakuwepo na kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa wanaokuja kupata huduma kwenye vituo vyao vya kutolea huduma.
Aliongeza kuwa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya unaendelea , Serikali ilitoa Bilion 1.5 na Bajeti ya juzi wameongeza milioni 500, vilevile kwa kipindi cha awamu hii ya nne ya uongozi Zahanati nne za Kijaka,Kigogo, Pembamnazi na Buyuni zimafanikiwa kuzinduliwa na kuanza kufanya kazi.
Mbunge aliongeza kuwa ili Kigamboni izidi kukua inahitaji wawekezaji na tayari watu wa Autralia wamegundua uwepo wa madini eneo la KisaraweII na kwamba kwa kulitambua hilo Serikali imetoa Milioni 90 kwaajili ya kuboresha miundombinu ya barabara itakayorahisisha usafirishaji.
Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri aliwashukuru watu wa Australia kwa kuikumbuka Kigamboni na kusema kuwa bado uhitaji wa magari ya wagonjwa upo , kwanye matarajio yao ya kuleta gari zingine 10 basi waikumbuke tena kigamboni hata kwa magari mawili.
Aidha kwa kipekee alimpongeza Mbunge Dkt.Faustine Ndungulile kwa kuipambania Kigamboni kwenye suala la afya ambapo hadi sasa ina jumla ya magari 5 ya kubebea wagonjwa , pia ametekeleza ahadi nyingi kwa wapiga kura na kwakupitia jitihada hizo wananchi wananufaika sana na Wilaya ya Kigamboni.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Arch.Ng’wilabuzu Ludigija amemshukuru Naibu waziri wa Afya na watu wa Australia kwa msaada walioutoa na kusema kwamba uhitaji bado ni mkubwa , kupatikana kwa gari hilo kutasaidia kuokoa maisha ya wananchi wa Kigamboni.
“Naibu waziri huyu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kigamboni tunamshukuru na anastahili kupongezwa anafanya kazi bila kuchoka na amekua msaada mkubwa kwetu, kwa niaba ya wananchi wa Kigamboni tunakushukuru kwa namna unavyoendelea kutupambania” Alisema Mkurugenzi
Australia Tanzania Society wanashirikiana na Wizara ya afya wazee jinsia na watoto kuboresha huduma za afya na hivi karibuni wanatarajia kuleta magari mengine 10 ya kubebea wagonjwa yatakayopelekwa maeneo mengine yenye uhitaji.
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni na Naibu waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndungulile akizungumza na watumishi na uongozi wa Kigam,boni kabla ya kukabidhi gari la wagonjwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri akishukuru Mbunge na Australia kwa msaada wa gari hilo na kuomba msaada wa kuongezewa gari 2 nyingine pale itakapowezekana.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Arch.Ng'wilabuzu ludigija akishukuru ubalozi wa Australia kwa msaada walioutoa kwenye hospitali ya Vijibweni
Viongozi wakishuhudia gari kwa muonekano wa ndani
Mwenyekiti wa Australia Tanzania society Bw. Didier Murcia akionesha muonekano wa gari hilo kwa ndani.
Muonekano wa gari kwa ndani
muonekano wa gari kwa nje
mwenyekiti wa Australia Tanzania society Bw. Didier Murcia akitoa maelekezo matumizi ya eneo la kuhifadhia oxygen
Naibu waziri wa Afya na Mbunge wa Kigamboni Dkt. Faustine Ndugulile akimshukuru mwenyekiti wa Australia Tanzania society Bw. Didier Murcia kwa msaada walioutoa Kigmaboni
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa