Waziri wa Viwanda,Biashara na uwekezaji Mh.Charles Mwijage ameagiza wakuu wa mikoa, wakurugenzi wa majiji na Halmashauri zote nchini kuandaa mpango utakaowawezesha kuwadhamini wakulima na hata watumishi katika mikoa na Halmashauri zao ili waweze kuwakopesha vifaa vya kilimo.
Waziri Mwijage amesema serikali imeagiza matrekta 250 kwa ajili ya kuwakopesha wakulima kote nchini na kwambani jukumu la Halmashauri kujua ni nani anastahili kukopeshwa na kusimamia urejeshaji wa mikopo hiyo.
Agizo hilo limetolewa alipokuwa akizindumaonesho ya nanenane kanda ya kati leo ambapo pia, Mh.Mwijage ameziomba taasisi za serikali zinazofanya kazi za udhibiti ubora kama TFDA,TBS ziwasaidie wazalishaji wakubwa na wadogo badala ya kuwafungia au kuwanyima vibali kama baadhi ya taasisi zinavyofanya.
“Nyie ndio jicho la serikali, muwasaidie wakulima na wafugaji kufikia malengo yao badala ya kuwakatisha tamaa” alisema Mh.Mwijage.
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ni mojawapo kati ya halmashauri sita katika mkoa wa Dar Es salaama ikiwa ni halmashauri kubwa kijografia ikiwa na ukubwa wa kilometa za mrabaShughuli kuu za kiuchumi za wananchi wa kigamboni ni biashara, uvuvi katika bahari ya Hindi , kilimo pamoja na ufugaji wa mifugo wa aina mbali mbali. Mifugo hii hufugwa katika njia mbali mbali za kisasa na za asili kulingana na eneo husika kwani mpaka sasa yapo baadhi ya maeneo ya Kigamboni yenye muonekano wa vijiji na hivyo kuruhusu watu kufuga kiasili. Mifugo inayofugwa ni kama vile ng’ombe, kuku, mbuzi, kondoo pamoja na samaki
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni inashiriki maonesho ya wakulima nane nane kwa mara ya pili tangu kuanzishwa kwake waka 2016, ambapo rai kubwa ni kuwahamasisha wananchi na wawekezaji kuja kuwekeza ndani ya ardhi ya Manispaa ya kigamboni kwasababu, kuna ardhi ya kutosha ya kuwekeza kwa maeneo ya viwanda, kilimo Mjini, maegesho ya magari na viwanja vya makazi.
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imeweza kuudhirishia umma kuwa kilimo mjini inawezekana kwani shughuli mbalimbali na mazao yaliooneshwa kustawi ndani ya ardhi ya Kigamboni kwenye maonesho ya wakulima nanenane mwaka 2018 imetoa fursa kwa wananchi kuwekeza ili kuendana na kauli mbiu ya mwaka 2018 ya "Wekeza katika Kilimo,Mifugo na Uvuvi kwa maendeleo ya viwanda".
Waziri wa Viwanda Mhe.Charles Mwaijage akihutubia wananchi kwenye ufunguzi wa maonesho ya wakulima nanenane Mkoani Morogoro.
wanafunzi wa shule ya wakiwa pamoja na mwalimu wao walipotembelea banda la Kigamboni Mc.
Waziri wa Viwanda Mhe.Charles Mwaijage akikagua moja ya banda la wakulima kabla ya kufungua maonesho ya wakulima nanenane Morogoro mwaka 2018
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mhe. Gulam Hussein Shaban Kifu akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Kigamboni kwenye maonesho ya nanenane, pembeni ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kigamboni Ndg.Stephen Katemba.
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mhe. Gulam Hussein Shaban Kifu akinunua bidhaa kutoka kwa wajasiliamali wa Kigamboni , alipotembelea banda la wajasiliamali kuona shughuli zinazofanyika.
wataalamu wa kilimo wakitoa elimu ya kilimo kwa wageni walifika kujionea shughuli za kilimo zinazofanywa na Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.
Zao la Bilinganya linavyostawi kwenye ardhi ya Kigamboni.
Watoto na wazazi waliofika kwenye banda la Kigamboni Kuona ufugaji wa kisasa wa samaki aina ya Sato
Baadhi ya mazao yanayostawi Manispaa ya Kigamboni.
mwananchi aliyetembelea banda la wajasilimali wa Manispaa ya Kigamboni akioneshwa bidhaa kablaya kuinunua.
Wanafunzi wa kidato cha kwanza kutoka morogoro waliofika kuona na kujifunza shughuli za kijasiliamali zinazofanywa na wananchi wa Kigamboni.
wanafunzi wakipewa elimu ya afya na mtaalam wa afya namna ambavyo mifugo inavyoweza kuepelea kuhatarisha afya zetu
Mtaalamu wa Kilimo akitoa elimu kwa wageni waliotembelea Banda la Kigamboni kwenye maonesho ya nanenane mwaka 2018
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa