Baraza la madiwani la Manispaa ya Kigamboni limewataka wataalamu kuongeza bidii kutafuta vyanzo vingine vya mapato ili kuisadia Manispaa kuweza kujiendesha na kufikisha huduma kwa jamii.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti leo kwenye mkutano wa kawaida wa robo ya pili ya baraza kwa mwaka 2018/2019 kilichofanyika kwenye ukumbi Wa Shule ya Mjimwema, Waheshimiwa Madiwani wamesema kuwa, vyanzo vingi tayari vinachukuliwa na serikali kuu, huku Manispaa ikiwa haina vyanzo vya kutosha vya kuingiza mapato hivyo kushauri kufikiri namna ya kuongeza mapato.
“Serikali kweli inachukua baadhi ya vyanzo vya mapato lakini mrejesho wake unaonekana mfano tumepata fedha za ujenzi wa hospitali ambayo itapandisha hadhi ya Wilaya, hivyo sioni kama kunatatizo, tunachopaswa ni kufikiri namna ya kupata vyanzo vipya vya mapato tutakavyoweza vimudu.” Alisema Mhe.Issa Zahoro
Aidha Diwani wa Kata ya Kibada Mhe. Amin Mzuri Sambo ameshauri waheshimiwa madiwani kusimama kwenye nafasi zao ili kuwapa nguvu watendaji katika kufanikisha lengo la kuinua mapato ya Manispaa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Arch.Ng’wilabuzu Ludigija amesema kwamba yeye pamoja na wataalamu wake wanapambana kuanisha na kuandika maandiko mbalimbali ya maeneo ya uwekezaji ikiwa pamoja na kutafuta wafadhili watakaowezesha kufadhili na kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali kama stendi,soko la samaki huku Manispaa ikipambana kuanzisha kiwanda cha kufyatua matofali, na kusema kuwa ushirikiano baina ya watendaji na Waheshimiwa Madiwani unahitajika kwasababu nia ni moja ya kunyanyua mapato sababu Manispaa haina kitu
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa