Diwani wa Kata ya Tungi na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Ernest Mafimbo amesema kuwa Manispaa ya Kigamboni imetumia zaidi ya Ths. Bilioni 2.7 ili kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mhe. Mwafimbo ameyasema hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani chenye lengo la kujadili Utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Manispaa katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2024/25
“Takribani Tsh. Bilioni 2.7 zimetumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi wa shule, mabweni, ujenzi jengo la dharula katika hospitali ya wilaya na uboreshwaji wa miundombinu mbalimbali ili kuleta maendeleo katika Manispaa yetu”
Aidha, Mhe. Mwafimbo amesema Manispaa ya Kigamboni imejipanga kuchukua hatua za dharula ili kudhibiti taka katika maeneo mbalimbali ili kuzuia magonjwa ya Mlipuko yanayoweza kutokea kutokana na mrundikano wa uchafu.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa