“Nawapongeza sana kwa kazi nzuri ,nimeona maendeleo ni mazuri hongereni sana kazi nzuri.”
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI (MB) Mhe. Selemani Jafo mapema leo katika ziara yake ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Nyumba za watumishi zinazo jengwa katika Mtaa wa Gezaulole, Kata ya Somangila.
Aidha katika ziara hiyo Mhe Jafo ametoa muda wa siku 20 hadi tarehe 1/1/2021 Nyumba hizo ziwe zimekamilika na ametoa wito kwa wataalamu wa Manispaa kusimamia kwa ukaribu ili watumishi waweze kuhamia.
Ujenzi wa nyumba za viongozi unahusisha nyumba 24 ikiwa ni agizo la Rais wa Jamhuri Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli alipofanya Ziara ya Kikazi ya uzinduzi wa wilaya na Manispaa ya Kigamboni Februari 2020.
Mkurugenzi wa Kigamboni Ndugu Erasto Kiwale akisoma taarifa ya Ujenzi, Nyumba za viongozi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Aboubakar Kunenge akipokea maeezo juu yautekelezaji wa Mradi
Waziri wa TAMISEMI Mhe Selemani Jaffo akitembelea na kukagua maendeleo ya Mradi
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa