Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Abubakar Kunenge leo amefanya ziara ya kukagua na kutembelea mradi wa ujenzi wa Nyumba 25 za viongozi zinazojengwa katika Mtaa wa Gezaulole Kata ya Somangila Manispaa ya Kigamboni.
Aidha katika ziara hiyo Mheshimiwa Kunenge ameupongeza uongozi wa Manispaa ya Kigamboni kwa kasi yake ya utekelezaji wa mradi huo na juhudi zake za kusimamia kwa ukaribu katika kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa muda uliopangwa.
Mradi wa ujenzi wa nyumba za viongozi unahusisha nyumba 25 amabapo nyumba 24 zinajengwa kwa gharama ya Tsh Bil 2. Ikiwa ni fedha zilizotolewa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli na Nyumba 1 inajengwa kwa Mapato ya ndani (Own Source) ambapo zinatarajia kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa