Na Joseph Semkiwa
Mwenyekiti wa kamati ya ushauri ya wilaya DCC ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Halima Bulembo ameupongeza uongozi wa Manispaa ya Kigamboni kwa kuzingatia hatua zote katika mchakato wa kutoa mapendekezo ya ugawawaji wa maeneo ya utawala (Kata na Mitaa)
Mheshimiwa Bulembo ametoa pongezi hizo leo tarehe 11/08/2023. Katika kikao cha ushauri cha Wilaya DCC kilichofanyika ili kupokea mapendekezo ya maeneo mapya ya utawala kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi yake kwa lengo la ya kusogeza huduma karibu zaidi kwa wananchi.
Aidha amesema kuanzishwa kwa maeneo mapya ya utawala kutasaidia kuharakisha maendeleo kwa haraka pia kutawaondolea adha wananchi kutembea umbali mrefu ili kufuata huduma muhimu.
Kwa upande mwingine Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mheshimiwa Faustine Ndugulile ameushauri uongozi wa Manispaa ya Kigamboni kulinda majina ya asili ya maeneo lengwa ili kuepuka mkanganyiko kwa Wananchi
Pia amewataka kuepuka makosa ya kimaandishi na ya uchapaji wa majina ya Kata na Mitaa mipya ili kuepuka makosa yasiyo ya lazima kwa hatua zinazofuata.
Sambamba na hilo akiwasilisha Mapendekezo hayo Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndugu Erasto Kiwale ameeleza kuwa mchakato ni shirikishi na ulianza katika ngazi ya Mtaa kabla ya kufika katika Kamati ya ushauri ya wilaya
Baadhi ya wajumbe walioshiriki katika kikao cha ushauri cha Wilaya DCC kilichofanyika kwa lengo la kupokea mapendekezo ya maeneo ya utawala
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mheshimiwa Halima Bulembo akiongea na Wajumbe
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndugu Erasto Kiwale akiwasilisha Mapendekezo
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa