Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imetwaa tuzo 3 za wadau wa usuluhishi kwa mwaka 2023 zilizotolewa na Jaji mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma katika ukumbi wa Mikutano wa Mwl Nyerere (JNICC) ulipo posta jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kuzikabidhi tuzo hizo kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Erasto Kiwale, Mkuu wa Kitengo cha huduma za Sheria Bi. Fortunata Shija amesema Manispaa imefakiniwa kupata tuzo 3 katika kundi la usuluhishi ambapo
Tuzo ya kwanza imetolewa kwa Halmashauri ya Manipaa ya Kgamboni kwa kuthamini Mchango wake wa kipekee katika uboreshaji Kiwango cha Mafanikio ya upatanishi kwa mwaka 2023
Tuzo ya pili imetolewa kwa Baraza la kata ya kibada kwa kuthamini Mchango wake wa kipekee katika uboreshaji Kiwango cha Mafanikio ya upatanishi kwa mwaka 2023.
Tuzo ya tatu imetolewa kwa Hamisi Mvugalo kwa kuthamini Mchango wake wa kipekee katika uboreshaji Kiwango cha Mafanikio ya upatanishi kwa mwaka 2023
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa