MSAADA WA VIFAA TIBA KUTOKA UJERUMANI KWA HOSPITALI ZA WILAYA MKOA WA DAR ES SALAAM, KIGAMBONI YANUFAIKA
Leo 4/2/2022 hospitali ya Wilaya ya Kigamboni imepokea vifaa tiba ( vitanda 24 na kabati zake 16) mara baada ya uzinduzi wa vifaa hivyo uliofanywa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.Amos Makalla ambae alikuwa ni mgeni rasmi aliezindua vifaa hivyo na kukabidhi Kwa Wilaya 5 za mkoa wa Dar es salaam.
Akiongea katika uzinduzi huo Mkuu wa mkoa amewashukuru wadau hao kutoka Hamburg Germany ambao Wana ushirikiano na Tanzania wa muda tangu mwaka 2007.
Aidha amesema kuwa msaada huo ni wa awamu ya kwanza ambapo kuna container nyingine itakuja inayoleta vifaa tiba vingine.
Kigamboni imenufaika Kwa kupewa vitanda 24 na kabati zake ndogo 16.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Almas Nyangasa Kigamboni amewashukuru wadau hao Kwa msaada huo kwani utasaidia kutatua upungufu uliokuwepo
Akiongea Meya Manispaa ameshukuru Kwa kupatikana vifaa hivyo kwani vinaenda kutatua changamoto iliyokuwepo ya uhaba wa vitanda.
Wilaya zingine zilizonufaika ni Ilala,kinondoni,Ubungo na Temeke Kwa kila Wilaya vitanda 21 na kabati ndogo 14.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa