MANISPAA YA KIGAMBONI YAPAA UKUSANYAJI MAPATO,TAMISEMI YAWAPONGEZA
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imeshika nafasi ya pili kwa Halmashauri za Manispaa zote nchini kwenye ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kigezo cha asilimia ya makusanyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serkali za Mitaa, Innocent Bashungwa (Mb) kuhusu Mapato na Matumizi ya Mapato ya Halmashauri zote 184 nchini kwa mwaka wa fedha 2021/2022 aliyoisoma jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti 2022, imeainisha kwamba Halmashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka husika ilipanga kukusanya shilingi bilioni 9,106,000,000 kupitia mapato yake ya ndani ambapo hadi kufikia mwezi Juni 2022 imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 10,761,334,792 sawa na asilimia 118.
Uchambuzi unaonesha kwamba, mwenendo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022, Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ni miongoni mwa Manispaa iliyokusanya mapato yake kwa zaidi ya asilimia 100.
Pongezi nyingi Sana ziwaendee Mkuu wa Wilaya ya kigamboni Mh.Fatma Almas Nyangasa,Meya wa Manispaa Mh.Ernest Mafimbo kwa usimamizi mzuri.Aidha Mkurugenzi wa Manispaa Ndg.Erasto Kiwale kwa utekekezaji wenye ufanisi pamoja na timu yake ya menejimenti.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Manispaa ya Kigamboni.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa