Aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndugu Stephen Katemba amewashukuru Baraza linalounda Madiwani, wakuu wa idara na watumishi wote kwa ushirikiano walioutoa kipindi cha uongozi wake na kuwaomba kuduudumisha kwa mkurugenz aliyekuja.
akizungumza kwenye makabidhiano ya Ofisi Ndg.Katemba amesema kuwa amefarijika kuwa mkurugenzi wa kwanza ndani ya Manispaa ya Kigamboni tangu kuanzishwa kwake na kwamba pale alipoishia anaamini pataendelezwa vyema na Mkurugenzi atakayeongoza kwa sasa.
"Wakuu wa Idara nawashukuru sana mmenifanya Rais azidi kuniamini na kuona bado ninaweza kumsaidia na kuendelea kulitumikia Taifa, naomba ushirikiano huu mlionipa uweze kukua zaidi kwa mkurugenzi huyu ambaye leo ninamkabidhi rasmi Halmashuri ya Manispaa ya Kigamboni" Alisema Ndugu Katemba.
Aidha Aliongeza kuwa ametenda vyema kazi na uongozi wa Meya akiwa anasaidiana na Naibu meya kwa mazuri na mabaya na mapungufu kwakuzingatia binadamu sio malaika lakini waliweza kuvumiliana na kufanya kazi vyema na kufikia mahali pazuri.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg.Ng''wilabuzu Ndatwa Ludigija alisema Serikali imewaamini na ili kuweza kutekeleza yale ambayo Mh.Rais na Serikali kwa ujumla wake yanapaswa kufanywa kwa wananchi ni vyema kudumisha ushirikiano baina ya watumishi,Waheshimiwa madiwani na uongozi wote wa manispaa na kwamba yupo tayari kufanya kazi wakati wote.
Naye Mkuuuwa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Sara Msafiri alitoa rai ya ushirikiano baoina ya uongozi wa Manispaa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili kuweza kuwahudumia wananchi vyema.
Makabidhiano yalifanyika kwenye ofisi za Mkurugenzi jana mara baada ya kushiriki kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa Kisaota Sekondari.
Ndg.Stephen Katemba akipeana mkono na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg.Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija (aliyeshika funguo), Meya wa Manispaa akishuhudia.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano kutoka kushoto ni Ndg.Stephen Katemba, Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe.Maabad Hoja, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg.Ng'wilabuzu Ndatwa
Picha ya pamoja baina ya viongozi, Afisa Utumishi na Mwanasheria wa Manispaa.
Baraza likiendelea
Baaadhi ya watumishi wakisikiliza kwenye kikao
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni akijitambulisha na kuzungumza kwenye Baraza lililofanyoika jana Ukumbi wa Kisota Sekondari
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa