Leo Novemba 6. 2024 Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kigamboni limeketi kwaajili ya kupitia na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali zilizofanywa na Manispaa katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mheshimiwa Ernest Mafimbo amesema Baraza limeiagiza Menejimenti ya Manispaa ya Kigamboni kufanya matengezo ya barabara muhimu katika Kata zote kabla ya kuanza kwa mradi wa DMDP ili wananchi waweze kusafiri kirahisi
Sambamba na hilo amesema Baraza limeiagiza Menejimenti kutafuta eneo kwaajili ya kujenga stendi ya Mabasi yanayoenda Mikoani ili wananchi wa Manispaa ya Kigamboni waweze kupata huduma ya usafiri kwa urahisi.
Kwa upande mwingine Mstahiki Meya huyo ameupongeza uongozo wa Manispaa kwa kufanya zoezi la upandaji na kutoa hati Milki kwa maeneo yote ya Umma yanayomilikiwa na Manispaa ili kuzuia uvamizi unaofanywa na baadhi ya Wananchi.
Aidha amesema katika robo ya kwanza Manispaa imejipanga kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ili yaweze kutumika kujenga miradi ya uwekezaji itakayowezesha pia kukuza Mapato
Hata hivyo alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha kwaajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo hususanikatika sekta ya Barabara
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa