"Naiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ipime eneo lote la Mbutu na ifuate taratibu na sheria zote za ardhi ili limilikiwe na Serikali pia litengwe kwaajili ya wachimbaji."
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu leo kwenye ziara yake aliyoifanya katika Mtaa wa Mbutu Kata ya Somangila Manispaa ya Kigamboni kwa lengo la kutembelea na kukagua eneo la machimbo ya vifusi vya Mawe, udongo na Kokoto.
Aidha Mheshimiwa Waziri alihitimisha ziara yake kwa kukutana na Wananchi wa Mtaa huo ambapo alisikiliza kero zao
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa