Manispaa ya Kigamboni kupitia Idara ya maendeleo ya jamii imeaandaa mafunzo maalumu ya vikundi vya huduma ndogo za kifedha ( VICOBA) kwa lengo la kuwajengea uwezo wanavikundi juu ya sheria na kanuni ya huduma ndogo za kifedha na kuwakumbusha umuhimu wa kusajiliwa.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo Agosti 29, 2023 katika ukumbi wa Kibada Garden uliopo kata ya kibada, mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Sigilinda Mdemu amesema kama idara waliona kuna haja ya kuandaa mafunzo hayo ili kuwapitisha viongozi na walimu wa VICOBA ili kujua sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa vikundi vya fedha.
"Tunataka wasajiliwe kwa sababu ni takwa la kisheria na ni kwa pande zote, vikundi vinapaswa kusajiliwa na walimu wanapaswa kuwa na leseni tumeona ni vyema viongozi wapate elimu hii ili waweze kuwa msaada kwenye vikundi hivyo," amesema Mdemu.
Amesema jumla ya viongozi 700 wamepatiwa mafunzo na kuelekezwa namna ya kusajili na kukata leseni kwa vikundi vyote ili kuweza kupata msaada wa kisheria pindi wanapopata changamoto.
" kikao hiki kitatoka na uwezeshaji wa umoja wa kifedha na jukwaa hili litapata fursa ya kusimamia mambo yao na kuzungumza kwa pamoja fursa zote za kifedha," ameongeza Mdemu.
Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Taifa Bi. Fatma Kange akitoa Salamu za Serikali amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Halima Bulembo kuwapatia eneo la ardhi ili litumike na kina mama kuendesha shughuli za maendeleo ikiwemo uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo huku wakihamasisha wajasiliamali kutengeneza bidhaa zenye ubora na zilizopatiwa usajili BRELA.
Naye Mjumbe wa kamati ya bodi KIWASA (Kigamboni Wanawake SACCOS) Bi. Meresiana Kimario amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa kwa kusimamia vyema ugawaji wa fedha za asilimia 10 za mapato ya ndani na akasema kuwa zimeongeza chachu katika kuwaletea maendeleo wanawake na kwa ustawi wa familia.
Jumla ya viongozi wa vikundi 243 wamepatiwa mafunzo hayo.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa