Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Almasi Nyangasa leo amefanya kikao kazi na wakuu wa Idara na vitengo, Watendaji wa Kata na Mitaa kwa lengo la kufahamiana lakini pia kuwekeana mikakati mizuri katika kuhakikisha lengo la Serikali linafikiwa.
Akizungumza na wataalamu hao kwenye ukumbi wa Manispaa Mhe. Fatma amesema kuwa kwanza angependa kuona ushirikianao unapewa kipaumbele katika kutekeleza majukumu ikiwemo kuona maeneo ya Mapato, Kero za wananchi, ulinzi na usalama, usafi pamoja na usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo (MKUUU) yanapewa kipaumbele.
Akizungumzia suala la ukusanyaji mapato Mhe. Fatma amesema kuwa ni vyema kuhakikisha vyanzo vyote vya mapato vilivyoainishwa vinakusanywa vizuri,kuongeza bidii ya kubuni vyanzo vipya vya mapato ambavyo vinaweza kuiongezea Manispaa Mapato,kuhakikisha mianya ya upotevu wa mapato yote inadhibitiwa kwa ukamilifu,pamoja na kudhibiti fedha za umma kwa kufanyi matumizi kwa kuzingatia taratibu na kanuni.
Kwa upande wa kushughulikia kero amewaasa Watendaji wa Kata na Mitaa kuepuka kuwa sehemu za migogoro na badala yake kuwa sehemu ya utatuzi kwa kusimamia haki,kuzingatia kufanya mikutano ya kisheria kwa ngazi za chini (Kata na Mitaa) na kutolea taarifa sahihi kwa wananchi.
Aidha amewataka Watendaji wa Kata na Mitaa kuhakikisha wanaainisha migogoro ya ardhi iliyopo kwenye maeneo yao kwa kuonesha chanzo na namna ambavyo wanapendekeza itatuliwe, kuandalia taarifa na kuipeleka ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Ameongeza kwa kuwataka maafisa utumishi kutatua kero za watumishi kwa kuwafata mahali walipo na kwakuanzia amewataka maafisa hao kushughulikia kero zinazowakabili waalimu.
Eneo la ulinzi na usalama Mkuu wa Wilaya amesema Watendaji wa Kata na Mitaa ndio watu muhimu katika kuhakikisha ulinzi na usalama upo katika maeneo yao hivyo ni vyema wakaimarisha vikundi vya ulinzi na usalama vilivyopo kwenye maeneo yao, nakuhakikisha wanasimamia na kudhibiti upitishwaji wa bidhaa za magendo kwenye maeneo yao na uhamiaji haramu.
Katika suala la usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo amesema ni muhimu kuhakikisha wananchi wanashirikishwa katika utekelezaji wa miradi kwa kuwapa uelewa wa kutosha na kuwafanya waone wao kuwa ni sehemu ya miradi iliyopo kwenye maeneo yao.
Watendaji wa Kata na Mitaa kuhamasisha wananchi wa Kigamboni kuhusiana na kujilinda kwa kuchukua tahadhari dhidi ya wimbi la tatu la ugonjwa wa korona.
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg. Erasto Kiwale amesema kuwa ,anaahidi kuhakikisha maelekezo yote yaliyotolewa kufanyiwa kazi kwa weredi na kwamba amefurahishwa na neno la mkuu wa wilaya kutaka kuwa sehemu ya maendeleo ya Kigamboni na kuhimiza ushirikiano jambo ambalo ni jema katika ufanisi wa kazi .
Baadhi ya watendaji wakifatilia maelekezo ya Mkuu wa Wilaya kwa makini.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Erasto Kiwale akipokea maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya na kumhakikishia utekekezaji kwa weredi.
Wataalamu wa Manispaa wakiendelea kuchukua maelekezo ya Mkuu wa Wilaya kwaajili ya utekelezaji.
Wataalamu wa Manispaa wakiendelea kufuatilia maelekezo ya Mkuu wa Wilaya.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa