“Naomba muwe na busara, hekima, uvumilivu, muwe makini na mfanye kazi kwa
weledi”
Wito huo umetolewa na Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kigamboni Ndugu,
Erasto Kiwale leo katika mafunzo yaliyohusisha makarani waongozaji wapiga kura
435 yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mwalimu Nyerere ili kuhakikisha
uchaguzi unafanyika kwa kufuata taratibu na sheria.
Aidha katika mafunzo hayo Ndugu Kiwale amesisitiza nidhamu wakati wa
kuwahudumia wapiga kura na kuwataka kuepuka kutoa kauli mbaya wakati wa
kipindi chote cha upigaji kura kwa kuzingatia makundi maalum ya Wazee
Wamama wajawazito na watu wenye ulemavu.
Uchaguzi mkuu wa Raisi Wabunge na Madiwani unatarajia kufanyika Siku ya
Jumatano tarehe 28/10/2020 ambapo utahusisha kata zote 9 za Manispaa ya
Kigamboni zenye vituo 417 vilivyopo katika Mitaa 67
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa