Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Hashim Mgandilwa amewaeleza wananchi waliofika kwenye Zoezi la utoaji dawa ya kutibu na Kuzuia Minyoo,Matende na Mabusha kuwa magonjwa hayo yanatibika tofauti na watu wengine wanavyodhani.
Mgandilwa ameyasema hayo katika Viwanja vya Navy Kigamboni ambapo uzinduzi huo ulifanyika Kimkoa kwa kushirikisha Halmashauri zote Sita za Mkoa wa Dar es salaam.
Zoezi hili linalosimamiwa na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto limezinduliwa leo tarehe 28/11 na litaendelea mpaka tarehe 3/12/2017 katika maeneo mbali mbali ambapo kwa upande wa Wilaya ya Kigamboni vituo 83 vimetengwa kwa ajili ya zoezi hilo.
Maeneo yaliyotengwa maalum kwa zoezi hili ni Hospitali ya Vijibweni,vituo vyote vya Afya na Zahanati za serikali na Binafsi ,Ofisi za kata ,Mitaa pamoja shule za msingi na sekondari.
Dawa hizi za kutibu na kuzuia Matende,Minyoo na Mabusha zinatolewa kwa watu wote wenye umri wa kuanzia Miaka mitano bila malipo yoyote.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Renatus Mchau amesema vituo vilivyoandaliwa vinatosha na pale patakapoonekana kuna uhitaji wa ziada ofisi yake itachukua hatua mara moja kwa kuongeza vituo ili kila mwananchi wa Kigamboni na wale wanakuja kupata huduma Kigamboni wanapata dawa.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa