Shirika lisilo la Kiserikali la JSI (John Snow Ink) leo limetoa mafunzo kwa wataalamu wa Manispaa na wadau mbalimbali juu ya programu ya uimarishaji wa mifumo ya Afya na ustawi wa jamii(GHSSP) unaotarajiwa kutekelezwa kwenye Kata tatu za Pemba mnazi,Kimbiji na Tungi yenye lengo la kupunguza maambukizi ya VVU (UNAIDS) la kufikia asilimia 90-90-90 kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.
Akizungumza wakati wa utoaji wa mafunzo hayo mkurugenzi wa Mradi kutoka JSI Bi.Pamela Msei amesema kuwa mradi umelenga kuwezesha upatikanaji wa huduma bora za afya na ustawi wa jamii kwa wanaoishi /walioathirika na VVUna makuni maalumu na ya kipaumbele.
Ameongeza kuwa lengo la kwanza ni kuwezesha uwepo wa rasilimli watu wenye ufanisi bora katika utoaji huduma za afya na ustawi wa jamii kwa WAVIU,WWKMH pili kuwa na miundombinu na mifumo ya kijamii inayofanya kazi na kuratibiwa vyema ili kuhudumia watu wenye mahitaji maalumu.
Mradi huu tayari unaendelea kwenye kata mbili za Kigamboni na Mjimwema.Kijiografia Mradi huu unatekelezwa kwenye Halmashauri 106 za Tanzania ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam Manispaa zote 5 zipo kwenye mradi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Maabad Hoja Akifungua mafunzo ya GHSSP
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Maabad Hoja Akifungua mafunzo ya GHSSP
Kaimu Mkurugenzi Bw.Edwin Owawa akitoa neno la ufunguzi wakati wa mafunzo
Muwezeshai kutoka shirika la JSI akifafanua mifumo itakayotumika kufikia lengo.
Baadhi ya watumishi na wadau waliopatiwa mafunzo hayo.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa