MADIWANI WA MJINI MAGHARIBI B WASHANGAZWA NA ENEO LA MACHINGA MANISPAA YA KIGAMBONI,WASEMA NI LA MFANO TANZANIA
Wakiwa katika siku ya pili ya ziara ya mafunzo hapa Manispaa ya Kigamboni Madiwani wa Mjini Magharibi B wamepata nafasi ya kutembelea eneo la machinga Manispaa ya kigamboni .
Wakiongea mara baada ya kupata maelezo ya eneo hilo lenye vibanda vya Machinga wamesema hawajawahi kuona eneo zuri la machinga kama hili Kwa hapa Tanzania hivyo wamepongeza uongozi wa Manispaa kwa hili na wameweka nia ya kuiga mfano huu watakaporudi kwao .
Eneo la machinga la Manispaa ya Kigamboni ni utekelezaji wa agizo la Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kuzitaka halmashauri zote kuhakikisha wanatenga maeneo rafiki kwa wamachinga ili wasikae katika maeneo yasiyo rasmi.
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imetekeleza suala Hilo kwa vitendo eneo hilo la kuvutia limesheheni vibanda vilivyo imara na katika mpangilio maalum wenye sehemu ya maduka,mama lishe,maduka,soko ,hongera Manispaa ya Kigamboni.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini KGMC
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa