MADIWANI MANISPAA YA KIGAMBONI WAFANYA ZIARA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
Hayo yamejiri 19/10/2022 ambapo Madiwani wa Manispaa ya Kigamboni wamekagua miradi 3 kwa lengo la kujionea utekelezaji wake .
Miradi hiyo ni ujenzi wa Soko la mazao linalojengwa katika kata ya Somangila ambapo mpaka kukamilika kwake jumla ya Tshs.milioni 90 zitatumika.Wakiongea katika majumuisho wajumbe wamehitaji kujua mikakati iliyopo katika kulitangaza soko hilo kwa kuwa lipo hatua za mwisho ambapo kaimu mkurugenzi ndg.Lawiso alieleza kuwa kupitia maafisa maendeleo ya jamii walioko Kata na kitengo cha Mawasiliano Serikalini utangazaji utafanyika ili kuwafikia wananchi licha ya hilo pia vikao vya awali vilifanyika kwa ngazi ya Kata na wananchi na wafanya biashara kuwajulisha,lakini pia utafanyika mpango wa kuhamishia mnada ambao huwa unafanyika Gezaulole kuhamia katika soko hilo jipya. Litakapokamilika soko hili litaiongezea halmashauri mapato kupitia ushuru utakaokuwa unalipwa na wafanyabiashara watakaokuwa wanatumia soko hili, pamoja na kusogeza huduma Kwa wananchi wa eneo hili ambao hawana huduma ya Soko.
Mradi mwingine waliotembelea ni mradi wa uuzaji wa viwanja eneo la Uvumba Kata ya Kibada ambapo Manispaa imepima viwanja 355 kwa matumizi mbalimbali viwanja hivyo vinatarajiwa kuuzwa mapema hivi karibuni ambapo wamepata maelezo ya taratibu zilizobaki ili sasa kuanza zoezi rasmi la kuuza viwanja hivyo kwa wananchi,mradi huu unatarajiwa kuiongezea mapato Manispaa hii.
Pamoja na miradi hiyo MADIWANI pia wametembelea eneo la Manispaa la shamba la Amadori lenye ukubwa wa ekari 2717,ambapo moja ya ushauri uliotolewa ni kufanyike mikakati kulipima eneo hilo na kuanza kufanya mikakati ya kuhakikisha miundo mbinu inayotakiwa inafanyiwa mipango ya kuwekwa.
Ukamilikaji wa miradi hiyo itaongeza tija katika kuongeza mapato ya Manispaa,lakini pia kuongeza huduma bora Kwa wananchi ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama Tawala CCM.Kazi iendelee.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini KGMC
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa