Baraza la Madiwani Manispaa ya Kigamboni likiongozwa na Mstahiki Meya Mhe.Erasto Mafimbo kwa pamoja limedhamiria kutoa ushirikiano wa dhati kwa wataalamu wa Manispaa kutekeleza shughuli za maenedeleo ikiwa ni pamoja na kushughulikia miundombinu korofi ambayo kwa namna moja imekua ikileta athari za mafuriko kipindi cha mvua.
Mstahiki Meya ameyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani kwa robo ya pili ya mwaka kwa lengo la kujadili taarifa za Kata na kuweka maazimio kwaajili ya utekelezaji.
Madiwani wamesema kuwa wamebaini changamoto ya mifereji katika Barabara ya Kibada kupitia Kisiwani hadi feri mitaro yake imeelekeza maji kwenda kumwagwa kwenye bwawa la chaboko ambalo pia hufurika kipindi cha mvua hivyo kuleta athali kwa wnanachi na hivyo kuona kunaumuhimu wa kushugulikia mapema suala hilo.
Kwa upande wa Dampo la Lingato Madiwani wameazimia kuwa dampo hilo litakapokuwa tayari lianze kutumika ili kuondoa adha ya kutokuwa na eneo maalumu la kutupia taka kwa wakazi wa Kigamboni.
Baraza la madiwani limeketi kwa siku mbili yaani tarehe 27-28 Januari ikiwa ni kikao cha pili kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Ernest Mafimbo akizungumza wakati wa kikao.
Baadhi ya Madiwani wakifatilia taarifa.
Madiwani wakifatilia taarifa
Wataalamu wa Mnispaa wakifatilia taarifa.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa