Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Manispa ya Kigamboni Ndg.Erasto Kiwale amewasisitiza wakufunzi kuzingatia miongozo, kanuni na sheria zinazoongoza utoaji wa mikopo ya asilimia 10% ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika mafunzo ili kuleta uelewa wa pamoja kwa Madiwani na watendaji wa Kata wanaopatiwa mafunzo hayo
Akizungumza wakati wa ufunguzi kwenye ukumbi wa Mikutano wa Manispaa, Mkurugenzi amesema kuwa wameona ni vyema kuandaa mafunzo hayo ili kuleta uwajibikaji wa pamoja kati ya wataalamu na Madiwani linapokuja suala la mikopo ya asilimia 10 ili kuondoa changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza
Aidha Mkurugenzi amesisitiza mafunzo kuwa shirikishi ikiwa ni pamoja na kujitahidi kuzingatia na kujielekeza kwenye mambo ya msingi.
Mafunzo haya ya Muongozo wa Manispaa wa utoaji na usimamizi wa mikopo ni ya siku moja na yamewalenga Watendaji wa Kata na Madiwani kwasababu ndio wanaoshiriki moja kwa moja na wananchi kwenye maeneo yao amabapo pia Maafisa maendeleo ya Jamii na Baadhi ya Wakuu wa Idara wameshiriki.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg. Erasto Kiwale akifungua mafunzo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Manispaa.
Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakifatilia mafunzo.
Waheshimiwa Madiwani wakifatilia Mafunzo
Watendaji wa Kata wakifatilia mafunzo
Baddhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Kata wakifatilia mafunzo
Baadhi ya Wakuu wa Idara wakifatilia mafunzo.
Mratibu wa Mikopo wa Manispaa ya Kigamboni Bi. Christine Ulaya akitoa mafunzo.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Happy Luteganya akitoa utangulizi wa mafunzo hayo.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa