MADIWANI MANISPAA YA KIGAMBONI WAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO
Katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa katika viwango vinavyotakiwa na kufuata utaratibu madiwani wa Manispaa ya Kigamboni wamefanya ziara kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo wametembelea miradi kadhaa kuona jinsi inavyotekelezwa.
Miradi iliyotembelewa ni mradi wa ujenzi wa bweni la wasichana,mradi wa ujenzi wa darasa kidete sekondari uliogharimu mil.20 ,ujenzi wa zahanati ya maweni,ujenzi wa madarasa 2 Minazini sekondari,pamoja na bwawa la chaboko.
Katika mradi wa ujenzi wa bweni ambao hadi kuisha kwake utagharimu kiasi cha shilingi mil.140 ambapo serikali kuu imetoa mil.80 na Manispaa mil.60 , hatua ya ujenzi upo katika umaliziaji .
Aidha mradi wa zahanati ya maweni itakayogharimu shilingi mil.120 hadi kukamilika kwake ujenzi ipo katika umaliziaji ambapo tayari madirisha yameshawekwa milango marumaru pamoja na rangi
Madarasa mawili yaliyopo Minazini yameshakamilika na tayari wanafunzi wanatumia madarasa hayo,ambapo gharama iliyotumika ni mil.40.
Akiongea katika Ziara hiyo Meya wa Manispaa ndg.Ernest Mafimbo ambae aliongoza ziara hiyo ameridhishwa na utekelezaji lakini pia katika eneo hatarishi lililotembelewa la bwawa la Chaboko madiwani wametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Manispaa kuwekwa kwa bicons katika eneo hilo ili kuzuia uvamizi usiendelee kwani ni eneo hatarishi linaloweza kusababisha maafa, pia kwa wale waliovamia na kujenga misingi wabomoe misingi hiyo ili kuepusha athari zinazotokana na mafuriko katika eneo hilo.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa