Baraza la Madiwani leo limemuagiza Mkurugenzi wa Manispaaya Kigamboni pamoja na timu ya mejimenti kuweka alama ya katazo ya uendeelezaji kwenye maeneo yote hatarishi na kuandaa michoro pamoja na kuandika andiko litakalosaidia kutafuta ufadhili utakaosaidia kujenga mkondo maalumu wenye nguvu ya kukusanya maji kuelekea baharini ili kunusuru Makazi ya watu yanayoathirika na maji yanayotawanyika kutoka kwenye bwawa la Boko linalochukua maji kuoka maeneo mbalimbali kuelekeza baharini
Akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza lililofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa Meya wa Kigamboni Mhe. Ernest Mafimbo amesema Mtaa wa Magogoni ni eneo ambalo linaathirika kwa asilimia kubwa kwani miundombinu ya kumwaga maji kutokea Daraja la Nyerere kueelekea baharini yanapita kwenye mkondo huo ambao unapita kwenye bwawa la boko lililopo kwenye mtaa huo hivyo kipindi cha mvua nyumba nyingi zinazungukwa na maji hivyo kusababisha athari za watu na makazi kutokana na utambalale wa mkondo huo.
Akizungumzia upande wa udhibiti wa maambukizi ya virusi vya Ukimwi Meya amesema wamewaagiza wataalamu kurejesha utaratibu wa kupanga ratiba ya kuonesha sinema za uelimishaji juu ya ukimwi, kuona athari na kupata tahadhari ya kujiepusha kwani janga hili bado lipo kwa kuangalia takwimu za kwenye vituo vyetu.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kimbiji Mhe. Sanya Bunaya amesema kuwa wananchi wamejishahu na kutumia njia ambazo sio sio sahihi za kujikiinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi na kuacha kufuata maelekekezo ya wataalamu ya namna bora ya kujikinga na maambukizi hali inayopelekea ongezeko la maambukizi hayo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigamboni Mhe. Yahaya Shabani amesema anashukuru kushiriki kikao cha Baraza la Madiwani kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake ameona kigamboni inaendelea kukua kwa kasi hivyo kwa kusikiliza hoja za wataalamu na Madiwani anaamini itaendelea kufunguka zaidi kimaendeleo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg.Erasto Kiwale amesema amepokea maelekezo yote na atashirikiana na timu ya menejimenti pamoja na wadau wengine ili kuhakikisha yanafanyiwa kazi kama yalivyoelekezwa kwa weredi.
Baraza la madiwani limejadiri pia taarifa za maendeleo za kamati mbalimbali ikiwa ni utaratibu wa kila mwisho wa robo ya kwanza kukamilika.
Baadhi ya Madiwani wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa taarifa za kila Kata Kwenye Mkutano wa Baraza robo ya kwanza uliofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa
Kutoka kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Ernest Mafimbo, katikatti ni Mwanasheria wa Manispaa ya Kigamboni ambaye kwa muda alishika nafasi ya mkurugenzi Ndg.CHarles Lawiso na mwisho ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Erasto Kiwale wakifuatilia uwasilishaji wa hoja mbalimbali wakati kikao cha Baraza kikiendelea.
Timu ya wajumbe wa menejimenti wa Manispaa ya kigamboni wakisikiliza kwa makini hoja zinazotolewa na madiwani kwenye mkutano wa baraza.
Timu ya wajumbe wa menejimenti wa Manispaa ya kigamboni wakisikiliza kwa makini hoja zinazotolewa na madiwani kwenye mkutano wa baraza.
Diwani wa Kata ya Kibada Mhe.Amini Sambo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kimaendeleo wa Kata ya Kibada.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Erasto Kiwale akifafanua baadhi ya Hoja zilizowasilishwa na Madiwani na kupokea baadhi ya maoni na maelekezo yaliyotolewa.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa