Manispaa ya Kigamboni imeshauriwa kuwa na miundombinu wezeshi ili kuwa wadau namba moja wa kudhibiti taka kwa kuelimisha wananchi na kuweka walau vihifadhi taka kwenye Mitaa ili kuwawezesha wananchi kutupa taka kwenye vifaa hivyo maalumu ili kulinda mazingira.
Hayo ameyazungumza muwezeshaji Baraka Thomas kutoka taasisi isiyokuwa ya kiserikali LEAT alipokuwa akitoa elimu ya mazingira kwa Mama lishe,Watendaji wa Kata na baadhi ya Mitaa na kusema kuwa, tukiacha mazingira yakaharibika kana kwamba hayatuhusu tutasababisha kizazi kijacho kushindwa kuishi vizuri sababu ya uharibifu wa mazingira unaofanywa leo hivyo ni vyema tukaonesha njia ili hata watoto wetu wajifunze kutoka kwetu.
Baraka alisema kuwa uzalishaji taka umegawanyika kwenye makundi mbalimbali kama Taka ngumu (solid waste), Taka za vimiminika (maji machafu),Taka za mfumo wa gesi, (mfano hewa za ukaa zinazalishwa viwandani),Taka hatarishi maranyingi zinaambatana na sumu mfano madawa vifaa vya mahospitali nk
Ameongeza kwa kusema kuwa Sheria ya mazingira inasema taka lazima zitenganishwe kwasababu makundi hayo yanatofautiana namna ya kudhibiti, kuzalishwa na kusafirishwa kwa kiwango kikubwa hivyo, ni vyema kuhakikisha tunadhibiti taka husasani taka ngumu na vimimika kwenye ngazi ya Kata na Mitaa, kwani zinaathari kubwa zikiachwa kuzagaa zagaa.
Aliendelea kwa kusema Watendaji wa Kata na Mitaa wakumbuke wanawajibu wa kuhakikisha taka zinazozalishwa kwenye maeneo yao zinadhibitiwa lakini pia wananchi kupewa uelewa wa umuhimu wa kutunza mazingira Ikiwa ni pamoja na kuzingatia kanuni ya tozo kwa kila anayezalisha taka na ndio maana sheria ndogo zimetungwa ili kusimamia usafi wa mazingira.
Aidha alisema, uteketezaji taka majumbani unafanywa kwa njia ambayo sio sahihi kulingana na magawanyo wa taka uliopo kwani sio kila taka zinatakiwa kuchomwa sababu baadhi moshi wake ni sumu, hivyo ni muhimu kuzingatia uteketezaji wa taka.
“Wananchi waelimishwe kuacha kuzalishaza taka ambazo hazina ulazima na kuchukua tahadhari kabla ya kuzalisha taka ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza jitokeza ”
Aliongeza kusema kadri watu wanavyoongezeka na uzalishaji wa taka unakua mkubwa hivyo tusipokuwa na mikakati ya kudhibiti taka, mazingira yetu yatakuwa machafu sana, kwani usafi wa mazingira unakupa nafasi ya utulivu, kuimarisha uwezo wa kufikiri hali inayopelekea kuwa na kizazi chenye nguvu, akili na afya.
Kwa upande wake Diwani wa Vijibweni Mhe. Zacharia Mkundi Alisema anashukuru kwa elimu iliyotolewa, lakini wamegusa sehemu tu ya Manispaa hivyo anapendekeza mradi huu kama ni wa muda mrefu ushuke ngazi za chini kabisa ili kuwe na uelewa wa pamoja mwisho wa siku lengo lililokusudiwa liweze kufikiwa..
Mafunzo hayo yalitolewa jana kwenye ukumbi wa G5 na taasisi isiyokuwa ya Kiserili inayofanya shughuli za ulinzi na uhifadhi mazingira na rasilimali za maliasili (LEAT) yaliyohusisha Kata za Kigamboni, Mjimwema,Tungi, Vijibweni, Kisarawe II na Kimbiji.
wataalamu kutoka Manispaa wakifatilia mafunzo
Diwani wa Kata ya Vijibweni Mhe. Zacharia Mkundi akishukuru LEAT kwa elimu waliyoitoa.
wataalamu ngazi ya Manispaa na wadau wengine wakifatilia mafunzo
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa