Kampuni ya Gas Entec toka nchini Korea Kusini imeonesha nia ya kujenga kiwanda cha kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati kitakachotengeneza meli za aina mbali mbali.
Mtendaji wa kampuni hiyo ndg Sang-Kuk Lee alifika katika ofisi za Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Kigamboni lengo likiwa ni kueleza mpango wao wa kuanzisha kiwanda hicho hapa nchini endapo serikali itakuwa tayari kuwapatia eneo katika fukwe za bahari ya Hindi zilizopo zilizopo Wilayani Kigamboni.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Sara Msafiri aliwahakikishia wawekezaji hao uwepo wa maeneo katika wilaya ya Kigamboni na hivyo kuwakaribisha kwa mikono miwili, na kusema kuwa uwepo wa kiwanda hicho utakuwa na umuhimu mkubwa wa ukuaji wa uchumi kwa Wilaya ya Kigamboni na nchi kwa ujumla kwani kitakuwa ni kiwanda cha kwanza cha aina hiyo kujengwa hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Ngw’ilabuzu Ludigija alisema ofisi yake iko tayari wakati wowote kuwapatia eneo la uwekezaji katika Manispaa yake.
“Sisi tunatekeleza kauli mbiu ya Mhe.Rais ya kujenga nchi ya uchumi wa viwanda hivyo kwetu sisi hii ni fursa muhimu sana” alisema Ndg Ludigija.
Baada ya uwasilishaji wa taarifa za pande zote mbili za Manispaa na wawekezaji , wawekezaji hao pamoja na wataalam kutoka idara mbali mbali waliambatana kwa pamoja kutembelea maeneo ambayo wawekezaji hao walioneshwa hatimaye kuafikiana na eneo la fukwe katika kata ya Pemba Mnazi ambapo walisema hatua itakayofuata ni kuwasilisha andiko la mradi ndani ya muda mfupi kuanzia sasa.
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ina eneo la fukwe lenye urefu wa kilomita 75 kuanzia eneo la Feri katika kata ya Kigamboni hadi Pembamnazi ambali linafaa kwa uwekezaji wa aina mbali mbali kama vile Viwanda,Hoteli na uvuvi.
Muwekezaji akitoa ufafanuzi wa namna watakavyo tekeleza mradi wao kwa uongozi wa Wilaya ya Kigamboni.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Sara Msafiri akiteta jambo na muwekezajiwawekezaji wakipitia mchoro wa ramamani kuona eneo la uwekezajiwawekezaji na uongozi wa Wilaya ya Kigamboni wakitembelaeeo fukwe PembamnaziPicha ya pamoja mara baada ya kutembelea eneo la pembamnazi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Arch.Ng'wilabuzu Ludigija akimkaribisha muwekezaji kuja kuwekeza eneo la fukwe Kata ya Pembamnazi.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa