Katika kutekeleza ilani ya chama na kuhakikisha huduma za afya zinakuwa bora kwa kila mwananchi Kituo cha Afya Kimbiji ni miongoni mwa vituo vya afya vilivyopokea fedha kutoka Serikali Kuu kwaajili ya Uboreshaji wa Huduma za Afya.
Uboreshaji wa Kituo hiki cha Afya umehusisha ujenzi wa jengo la upasuaji, maabara, jengo la kuhifadhia maiti, jengo la mama na mtoto ambapo hadi kukamilika kwake imegharimu kiasi cha Tsh. 514,429,38. Serikali Kuu imetoa kiasi cha Milioni 400 na Manispaa imechangia kiasi cha Milioni 114.4
Kukamilika kwa mradi kunaenda kusaidia wananchi wa Kimbiji na maeneo ya jirani kutokutembea umbali mrefu kufata huduma za Afya, kuokoa maisha ya mama na mtoto, na kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa ujumla kwa maeneo yote yanayozunguka Kata ya Kimbiji.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Dkt. Charles Mkombachepa amesema kuwa Kituo cha Afya Kimbiji kimekamilika kwa asilimia 100 na huduma zote zinatolewa ambapo hadi mwanzoni mwa Oktoba operation tatu za henia, mama wajawazito wawili zimefanyika na kuonesha matokeo chanya.
"Ijumaa tarehe 4/10/2019 tumefanikiwa kufanya operation mbili za wamama wajawazito na wote wametoka salama pamoja na watoto wao"
alisema Mganga Mkuu.
Jengo la mama na mtoto
muonekano wa ndani wa wodi ya mama na mtoto
Jengo la chumba cha upasuaji
muonekano wa ndani kwenye chumba cha upasuaji
majengo pacha ya maabara na upasuaji
muonekano wa ndani wa maabara
Chumba cha kuhifadhia maiti
Majengo ya awali ya utoaji wa huduma kwenye kituoa cha afya kimbiji kabla ya maboresho
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa