Kila mwananchi wa Kigamboni afahamu kuwa suala la usafi ni wajibu wa kila mtu, Tujitokeze kufanya usafi wa jumla kwani maeneo yote tunayofanya usafi tunayatumia.DC FATMA.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Almasi Nyangassa ambaye ameongoza zoezi la usafi leo amesema, zoezi la usafi ni endelevu kuhakikisha Dar es Salaam inapendeza kama kauli mbiu yake inavyosema PENDEZESHA DAR ES SALAAM na Kigamboni inaendelea kuwa safi kwa kauli mbiu ya KIGAMBONI SAFI WAJIBU WANGU hivyo, kila mtu kwa nafasi yake iwe eneo la makazi, biashara au umma wote tunawajibika kuhakikisha ni masafi.
Mkuu wa Wilaya amesema kila mtu aone anawajibika kushiriki kwenye usafi wa jumla na lakini kuhakikisha eneo lake linakuwa safi kwani tukienda na mwenendo huu itarahisisha mwisho wa siku kutotumia muda mwingi kwenye usafi wa jumla bali kujiridhisha tu, kwani usafi unakuwa umekwisha fanyika.
Ameongeza kuwa iwe kwa mfanyabiashara au sio, hakikisha eneo unalotumia ni safi na taka unazozalisha zinahifadhiwa na kuteketezwa vizuri kwenye eneo husika, hivyo amewaagiza Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa kusimamia ili kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa na iwapo kunaikuikwaji wowote kuchukua hatua kwa kutumia sheria ndogondogo zinazoiongoza Manispaa.
“Tupo tayari kuchukua hatua stahiki kwa yeyote atakayekaidi, kwa sasa tunazungumza kirafiki kwasababu wewe ni mwananchi wetu ,hivyo timiza wajibu wako kuhakikisha mazingira yanakuwa safi” Alisema Mhe.Fatma.
Akiongelea kuhusu usafi wa Fukwe Mhe. Fatma amesema Fukwe ni fedha na ni uchumi hivyo amewaomba wananchi wanaofanya shughui zao kwenye maeneo hayo na wanaojipumzisha kuhakikisha wanaweka mazingira safi mbali na mkakati uliopo ambao kama Serikali wamejipanga kuhakikisha fukwe zote zinakua safi.
Aidha amewataka wafanyabiashara wote wanaofanya biashara maeneo yasiyo rasmi kurejea kwenye maeneo yao waliyopangiwa na iwapo kunachangamoto zinazowakwamisha wawe tayari kuzifikisha ofisini ili zifanyiwe kazi kuliko kurejea kwenye maeneo ambayo tayari yamekatazwa kufanya biashara.
“Nirudie tena ni Marufuku kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi na yanafahamika”. Mhe. Fatma alisema
Madereva wa dalala dala pia wametakiwa kudhibiti utupaji taka hovyo hasa maeneo ya Barabarani kwa kuweka vitenga vya kuwekea taka ndani ya magari yao kuwezesha abiria kuzihifadhi humo.
Usafi wa Jumla wa mwisho wa mwezi huu wa kuminamoja umefanyika kwenye maeneo yote ya Barabara kuu za Kigamboni na maeneo yote ya Kata na Mitaa.
#KIGAMBONI SAFI, WAJIBU WANGU
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Almasi Nyangassa kulia na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg.Erasto Kiwale wakishirikiana kukusanya taka ili kuzihifadhi kwenye kifaa maalumu baada ya kuzikusanya.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Fatma Almasi Nyangassa akishirikiana na baadhi ya wananchi kwenye zoezi la ukusanyaji taka na kuzihifadhi kwenye chombo maalumu.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kufanya usafi wakisafisha mitaro ya barabara eneo la feri Kigamboni.
Zoezi la usafi likiendelea huku viongozi mbalimbali wakishiriki kwa kuongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Fatma Almasi Nyangassa.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kufanya usafi wakikusanya taka hizo na kuzihifadhi kwenye kifaa maalumu cha kukusanyia taka.
Mkuu wa Wilaya Mhe. Fatma Almasi Nyangassa akiwa ameambatana na mdau wa mazingira wakihifadhi taka kwenye chombo maalumu kilichowekwa mara baada ya kuzikusanya.
Mwananchi akikusanya taka kwaajili ya kuzipeleka sehemu maalumu ya kuhifadhia baada ya kufanya usafi.
Mandhari za barabara mara baada ya kufanyiwa usafi.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa