*RC MAKALLA AMSHUKURU RAIS SAMIA KUTOA FEDHA UJENZI WA MADARASA 618*
-Asema *Mkoa umepokea Bilioni 12 na milioni 360 kwa ajili ya Ujenzi huo*
- Aelekeza *Ujenzi wa vyumba vya madarasa ufanyike kwa Force Account*
- Ataka *Ujenzi kuzingatia Ubora, thamani ya pesa na kukamilika kwa wakati*
*RC Makalla* amesema hayo leo *Octoba 7,2022* katika kikao chake na Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari DSM, Ukumbi wa Arnatoglo Mnazimmoja, ambacho *kilihudhuliwa na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Maafisa Elimu, na Sekretarieti ya Mkoa* ikiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo *Bi Rehema Madenge*
*Mhe Makalla* amemshukuru *Rais Samia Suluhu Hassan* kwa kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo kufuatia Mkoa huo kupewa kiasi cha Bilioni *12 na milioni 360* ambazo zimeelekezwa katika Ujenzi wa vyumba vya *madarasa 618* sawa na *shule 108*
Aidha *RC Makalla* ameelekeza kujenga Madarasa ya mfano kwa kutumia *Force Account* huku akisisitiza pesa hizo zikatumike kujenga madarasa na sio kulipa fidia.
Vilevile *Mhe Makalla* amewataka kusimamia vizuri zoezi hilo kwa kuzingatia *thamani ya pesa na Ubora* bila kusahau kazi ifanyike kwa wakati *ifikapo Novemba 30,2022* Ujenzi uwe umekamilika.
Sambamba na hilo *RC Makalla* amesema amepokea *migogoro 41shule za Sekondari na 25 Shule za msingi* ya uvamizi wa Ardhi maeneo ya shule hivyo amewataka *Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi* kwenda kumaliza migogoro hiyo kwa kuyatembelea maeneo hayo, *kuyakagua, Kuyajua vizuri maeneo hayo na kuweka mipaka*
*RC Makalla ameelekeza migogoro yote ikashughulikiwe kwa ufanisi na apatiwe taarifa ya Utekelezaji wa zoezi hilo*
Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni *Mhe Godwin Gondwe* kwa niaba ya wakuu wa Wilaya wengine amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kwenda kutekeleza maagizo yake aliyotoa ili ifikapo *Januari 2023* wanafunzi waingie katika vyumba hivyo vya madarasa.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa