KAMATI KUU KANDA YA MASHARIKI CHAFANYA KIKAO CHA PILI CHA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA NANENANE 2022
Kamati Kuu Kanda ya Mashariki ya maonesho ya Nanenane Leo hii 15/7/2022 imefanya kikao cha pili cha maandalizi ya maadhimisho kwa 2022. Hayo yamejiri Leo 15/7/2022 katika Ukumbi wa JKT uliopo Viwanja vya nanenane Morogoro.
Akifungua kikao mwakilishi wa Mwenyekiti wa kikao hicho Mh Malima wa Mkoa wa Tanga amewakaribisha wajumbe na kuwashukuru kwa kuja Kisha kuwakaribisha sekretarieti kwa ajili ya kuzipitia na kujadili agenda za kikao.
Kikao hicho kilihusisha agenda kadhaa kwa ajili ya maandalizi ikiwepo agenda ya taarifa ya Maandalizi na Bajeti ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki 2022.
Kwa mwongozo wa Mwenyekiti bajeti ilipitiwa na kujadiliwa kwa kina na kufanya maamuzi.
Aidha Kamati ilipata nafasi ya kutembelea mabanda yote ya halmashauri za Kanda hii ili kujionea hali halisi ya maandalizi ikiwepo vipando .
Pamoja na hilo pia imeagizwa Maafisa Habari wa Halmashauri kuhusishwa katika kamati ya habari ya maandalizi ya nanenane.
Aidha imeshauriwa maafisa habari wa halmashauri kuanza uhamasishaji wananchi kushiriki maonesho katika viwanja vya Nanenane Morogoro.
Akifunga kikao Mwenyekiti amezitaka halmashauri kufanya ukaguzi wa vipando vyao katika mabanda Yao hapa viwanja vya Nanenane Morogoro na kila halmashauri ijipime na halmashauri nyingine ili kuboresha ili yawe katika hali njema pia kufanya maandalizi ya vikundi vya wakulima na mifugo.
Maadhimisho haya yamerejeshwa tena na serikali ya awamu ya sita ambapo 2021 hayakufanyika yataadhimishwa 8/8/2022.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO MANISPAA YA KIGAMBONI
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa