Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri ameshukuru uongozi wa CRDB Benki kwa kukubali ombi la kuwawezesha wajasiliamali walio na vitambulisho vya ujasiliamali kwa kusaini mkataba utaowawezesha kutumia vitambulisho vyao kuwa dhamana ya kupata mikopo ili kuinua uchumi wao.
Akizungumza leo kwenye ukumbi wa mkutano ofisini kwake Gezaulole, Mhe Sara amesema kuwa anayofuraha kuwa Kigamboni iliweza kutoa vitambulisho kwa wajasiliamali 22elfu na kwamba mfumo wa kitakwimu wa kuwatambua wafanyabiashara wote, mahali walipo na shughuli wanazofanya umefanyika ambapo kwa kuanza wajasiliamali 3042 wataanza kupata mikopo kwenye uzinduzi wa awamu ya kwanza na kiasi cha Bilioni 10 zimetengwa kwaajili yao.
Mkuu wa Wilaya amesema kuwa Rais alilenga kutoa vitambulisho hivyo ili kuwajengea uwezo wafanyabiashara wadogo kuweza kutoa huduma kwenye miradi mikubwa ya kimkakati ambapo Kigamboni imeamua kutumia fursa hiyo ya kukipa thamani kitambulisho kwa kutumika kama dhamana ya kukopa ili kufikia lengo la Rais la kuwakwamua kiuchumi wananchi na wafanyabishara wadogowadogo ambao walikuwa hawawezi kukopesheka bila kuwa na dhamana za uhakika.
“Tunaishukuru CRDB kwa kukubali ombi letu na kuamua kuanza na Kigamboni , niwahakikishie hii mbegu mnayoipanda haitafutika na wajasiliamali wetu hawatawaangusha” Alisema Mkuu wa Wilaya
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kigamboni Ng’wilabuzu Ludigija amesema kuwa Ubunifu wa Vitambulisho hivi vya Rais leo unaleta matokeo chanya kwakua lengo kuu lilikua ni kuwawezesha wafanyabiashara ambapo Kigamboni imeweza kuvipa thamani kuwa dhamana ya kupata mikopo na kwamba CRDB itawezesha kuwakopesha wajasiliamali kwa kima cha chini kuanzia 10,000 hadi 500,000.
Ameongeza kuwa huu ni ukombozi mkubwa kwa wajasiliamali na katika safari ya kuelekea uchumi wa kati hawataki kumuacha mtu hata mmoja ndiomaana kitambulisho hicho kitawawezesha kupata huduma za kifedha na kwamba anaipongeza CRDB Benki kwa ubunifu wa kutumia fursa hiyo ambayo itakua ni mfano kwa benki nyingine .
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Benki Abdul Majid Nsekela amesema kuwa anampongeza Mkuu wa Wilaya na watendaji wake kwa ubunifu wa kuona namna bora yakukipa thamani kitambulisho cha mfanyabiashara ili kumkuza mjasiliamali mdogo katika kufikia uchumi wa kati.
Ameongeza kuwa CRDB ni Benki ya wote na kupitia Kigamboni huduma hii itasambaa nchi nzima hivyo CRDB ipo tayari kuwahudumia wafanyabiashara wadogo ambao kwa kundi kubwa ni wamachinga na kwamba kwa kushirikiana na watendaji wa Manispaa hadi sasa wameweza kusajili wajasiliamali 3000 kutoka makundi balimbali.
“Safari ya kuboresha maendeleo ya wajasiliamali inaanzia Kigamboni ,tunatarajia Benki yetu itawafikia na kuwawezesha wafanyabiashara kwa mitaji, elimu na uwekezaji kwa vikundi na mtu mmoja mmoja kwa kupata huduma bora kwa urahisi na wakati wote na sasa tupo kwenye utoaji wa elimu ili kuwawezesha biashara zao kukua” Alisema Mkurugenzi wa CRDB Benki.
Mkurugenzi amesema kuwa wameamua kutumia mfumo wa kidigitali ili kuweza kuwafikia wajasiliamali wengi kwa kutumia mfumo wa simu akaunti ambao ni rahisi na hauna gharama katika utumiaji wake na kwamba CRDB imejipanga kuwahudumia ili kuwatoa kwenye hatua moja kwenda nyingine.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Benki Ndg.Abdul Majid Nsekela kushoto na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Arch. Ngw'ilabuzu Ludigija wakisaini mkataba wa kuwawezesha wajasiliamali wa Kigamboni leo kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya Gezaulole.
Mkurugenzi wa CRDB Benki kushoto Abdul Majid Nsekela akipeana mkono na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni kuashiria ushirikiano wao mara baada ya kuweka saini mkataba wa kuwezesha wajasiliamali wadogo
Mkurugenzi wa CRDB Benki Abdul Majid Nsekela akizungumza namna CRDB ilivyojipanga kuhakikisha huduma bora zinatolewa leo kwenye utiaji wa saini ya mkataba wa kuwezesha wajasiliamali
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri akizungumza kabla ya utiaji wa saini mkataba wa kuwezesha wajasilimali wadogo wa Kigamboni
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Arch.Ng'wilabuzu Ludigija akizungumza namna ambavyo vitambulisho vya wajasilimali vinakua mkombozi katika kuelekea uchumi wa kati
Picha ya pamoja na viongozi kutoka CRDB Benki na Wilaya ya Kigamboni mara baada ya kusaini mkataba
Baadhi ya watendaji wa CDRB na Manispaa ya Kigamboni
Baadhi ya watendaji wa Manispaa
baadhi ya watendaji wa Wilaya
Picha ya pamoja na wawakilishi wa wajasilimali na viongozi mara baada ya kusaini mkataba
Picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki Miliki©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa