Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imepongezwa kwa kupata hati safi kwa miaka miwili mfululizo na kutakiwa kuchukulia pongezi hizo kama hamasa ya kufanya vizuri zaidi.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkaguzi kutoka ofisi ya CAG Bw. Pastory Massawe wakati wa kikao maalum cha baraza la madiwani kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Sunrise Hotel kwa ajili ya kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa Fedha za serikali (CAG).
Mkaguzi Wa hoja za Serikali amesema kuwa ili kuendelea kupata hati safi ni vyema sheria na taratibu zikafuatwa ikiwemo wakuu Wa idara na Vitengo kuhakikisha wanatoa ushirikiano Wa kutosha pindi nyaraka zinapohitajika kwaajili ya kufuta hoja ambazo hazinaulazima Wa kuwepo na kabla ya kuingia kwenye hatua ya menejimenti.
"Wakuu wa Idara suala la hoja si vyema kuwaachia wasaidizi wenu na hata mkiwaachia hakikisheni majibu yaliyotolewa mmejiridhisha nayo kabla ya kulabidhi Kwa Mkaguzi " Alisema Mkaguzi Pastory
Aidha Mkaguzi ametoa rai Kwa waheshimiwa madiwani na watendaji kudumisha ushirikiano na wakuguzi, na kujipanga vizuri kwenye kipindi cha Ukaguzi ili kusaidia kuondoa hoja.
Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Maabad Hoja amemshukuru Mkaguzi Pastory na kuahidi Kwa niaba ya madiwani kutoa ushirikiano pindi itakapobidi ili kuendeleza upatikanaji wa Hati safi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni Arch.Ng'wilabuzu Ludigija amemshukuru Mkaguzi na uongozi Wa Mkoa Kwa ushauri na maoni waliyoyatoa na kuahidi kusimamia sheria taratibu na kanuni katika kuhakikisha hoja zinapunguzwa na kuendelea kushikilia hati safi.
Akiwasilisha taarifa ya Halmashauri kwa niaba ya Mkurugenzi Mweka Hazina wa Manispaa ya Kigamboni Ulinyelusya Mwamtobe amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 halmashauri ilikuwa na hoja 27 ambapo baada ya majibu kuwasilishwa na uhakiki kufanyika hoja 5 zilipendekezwa kufungwa na kusalia na hoja 22 ambazo zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na uhakiki utafanyika wakati wa ukaguzi wa mwaka 2018/2019.
baadhi ya wakuu wa idara wa Manispaa
Mwekahazina wa Manispaa Ulinyelusya Mwamtobe akiwasilisha taarifa ya fedha kwa niaba ya mkurugenzi.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa