Uongozi wa Kigamboni umepongezwa kwa kusimamia vizuri fedha za Serikali na ukusanyaji wa mapato hali iliyopelekea kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo.
Pongezi hizo zimetolewa na Bw.Suleiman Mwaliwale Mkaguzi wa nje wa Hesabu za Serikali za mitaa Jana kwenye Baraza maalumu la hoja kwa mwaka wa fedha 2018/2019 lililofanyika kwenye ofisi za Mkurugenzi.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Bi. Marry Assey kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa amesema ili kuendelea kufanya vizuri ni vyema kila Idara isimame kwenye nafasi yake na kuepuka maswali yatakayopelekea hoja kwakuwa na vielelezo sahihi pindi wakaguzi watakapofika kukagua.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa