Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Sara Msafiri amempongeza Mganga Mkuu wa Wilaya na Idara nzima ya afya kwa kufanikisha kuvuka lengo la utoaji wa chanjo ya Surua Rubella na Polio iliyofanyika tarehe 17-21 Oktoba ambapo Kigamboni imeongoza kwa Mkoa mzima wa Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kikao cha kupokea mrejesho wa zoezi hilo leo kwenye ukumbi wa ofisi uliopo Gezaulole, Mkuu wa Wilaya amesema mbinu walizotumia Idara ya afya kuhakikisha walengwa wote wanafikiwa ni vyema na matukio mengine yanayohusu jamii moja kwa moja zitumike.
Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt.Charles Mkombachepa amesema kuwa katika zoezi hilo la utoaji chanjo Wilaya ilitarajia kuchanja watoto 26711 wa Surua Rubella lakini wamechanja watoto 34366 sawa na asilimia 129% na watoto waliotarajiwa kupata chanjo ya Polio ni 15281 lakini wamefanikiwa kutoa chanjo kwa watoto 19,523 sawa na asilimia 128 ambapo jumla ya vituo 25 vilitoa huduma hizo.
Mganga Mkuu amesema kuwa mbali na changamoto ya mvua lakini waliweza kutumia mbinu za kupita nyumba kwa nyumba kuhamasisha wananchi kwa kutumia viongozi wa mashina ya chama cha CCM, matangazo ya bodaboda na gari na kuhamisha vituo vya kutolea chanjo kwenda kwenye ofisi za mitaa ndizozilizosaidia kuvuka lengo na kuipatia Kigamboni nafasi ya kwanza ya utoaji chanjo.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa