*RC MAKALLA: DSM IMEFANYA VIZURI MKATABA WA LISHE*.
- Awapongeza *Maafisa Lishe kwa kufuta rekodi mbaya ya lishe iliyokuwepo.*
- Awaelekeza *Wakurugenzi kuwawezesha Maafisa Lishe kutekeleza Majukumu yao na kutoa fedha kwa wakati*.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe Amos Makalla* amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo *kuwawezesha Maafisa Lishe* kutekeleza Majukumu yao na sio kuwaona hawana kazi kwa kuwageuza kuwa watu wa *kuisaidia kwenye matukio ya dharura* hususani *Kamati za chakula* kwenye mikutano.
*RC Makalla* ametoa maelekezo hayo wakati wa *kikao Cha tathimini ya utekelezaji wa mkataba wa Lishe* ambapo amewapongeza *Maafisa Lishe* kwa kazi kubwa waliyoifanya kufuta *tatizo la Lishe duni* lililokuwa likiikabili Dar es salaam.
Aidha *RC Makalla* ameelekeza Halmashauri *kutoa fedha za utekelezaji wa Lishe kwa wakati* muafaka ili kuwezesha *Maafisa Lishe kutekeleza Majukumu yao* tofauti na Sasa ambapo *pesa inatoka kwa kuchelewa*.
Katika kikao hicho *RC Makalla* ametoa zawadi ya vyeti kwa *Halmashauri zilizofanya vizuri kwenye suala la Lishe* ambapo *Manispaa ya Kigamboni* imeshika *nafasi ya kwanza* ikifuatiwa na *Halmashauri Temeke* iliyoshika nafasi ya pili na *Halmashauri ya Kinondoni* nafasi ya Tatu.
Itakumbukwa kuwa *Rais Samia Suluhu Hassan* kipindi Akiwa *Makamu wa Rais* aliingia mikataba na *Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanaondoa athari za utapiamlo katika maeneo yao.*
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa