Hayo yamebainishwa 9/3/2022 na Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na biashara Mhe.Dkt.Ashatu Kijaji katika ukumbi wa Wilaya ya Kigamboni wakati wa tukio la kusaini mkataba wa mauziano ya eneo la square mita za mraba mil.2.2 lililopo Kisarawe II Kigamboni Kwa ajili ya uwekezaji mkubwa wa Kongani ya Viwanda ambao haujawahi kutokea Kati ya property international na kampuni ya Elsewedy ya Egypt.
Akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini mkataba wa mauziano ili utekelezaji wa mradi uanze Mhe.Dkt.Ashatu Kijaji amesema mafanikio hayo ya mchakato wa kuanza kutekelezwa Kwa mradi huo ni matokeo ya jitihada za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan ambapo amekuwa akiifungua Tanzania kiuchumi toka aingie madarakani.
Aidha amesema mradi huu unaenda kuifanya kigamboni kuwa tajiri kutokana na mapato yatakayopatikana kutoka katika Viwanda vitakavyowekezwa katika eneo hilo ikiwepo Viwanda vya nguo,Viwanda vya kuunganisha magari ,kiwanda cha madawa ambapo tayari mwekezaji wa kiwanda cha madawa ameshasaini mkataba na Elsewedy Kwa ajili ya kuja kuwekeza katika eneo hili ,pamoja na hayo fursa za ajira zitakazopatikana Kwa uwekezaji huu ni ajira 50,000.
Mhe Waziri amewataka watendaji kujiandaa na kazi hiyo njema na wananchi wafanye jitihada kuchukua fursa hii adimu kwani ni fursa ya uhakika Kwa kuwa tayari masoko ya uwekezaji huu yapo nje ya nchi Jambo ambalo litaiingizia nchi yetu fedha za kigeni.
Kwa upande wa miundo mbinu rafiki kuelekea eneo la mradi amesema serikali tayari imetenga fedha Kwa ajili ya kujenga barabara ya lami ya kilometa 11 kutoka Kibada mpaka eneo la mradi Kisarawe II na utekelezaji utaanza mara moja ili Kurahisisha utekelezaji wa mradi.
Nae katibu Mkuu wa Uwekezaji, Viwanda na biashara Prof.Godius Kahyarara katika hafla hiyo amewashukuru timu nzima iliyohusika katika kufanikisha mchakato huu hadi kufanikiwa wakiwepo wanasheria wa pande zote mbili na Property International.
Aidha ameahidi kutoa Afisa katika ofisi yake atakaekuwa akifuatilia utekelezaji wa mradi huu kila siku mpaka kukamilika kwake ambapo amesema mradi utakamilika ndani ya miaka 2 .
Licha ya kuzungumzia manufaa mengi ya mradi huu Mhe.Fatma Almas Nyangasa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Rais Samia Suluhu Hassan Kwa maono yake ya kuifanya Tanzania yenye maendeleo kiuchumi na jitihada zake za kuifungua nchi kiuchumi na kuwaletea maendeleo watanzania na tupo tayari kumuunga mkono Rais katika jitihada za kuiletea nchi maendeleo,akizungumzia kunufaika Kwa wanakigamboni na wananchi Kwa ujumla amesema wingi wa ajira Kwa vijana ,kuongezeka kwa mapato kutokana na Kodi amegusia pia faida itakayopatikana Kwa wanakigamboni kutoka Kwa wawekezaji kusaidia jamii(CSR)Kwa kurudisha faida Kwa jamii.Pia amewashukuru wote waliohusika na kushirikiana nao tangu kuanza Kwa mchakato huu , shukrani Kwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na biashara Mhe.Ashatu K.Kijaji, Katibu Mkuu wa Uwekezaji,Viwanda na biashara Prof.Godius Kahyarara na Property international.
Akifunga hafla hiyo Kwa kutoa shukrani Mhe.Ernest Mafimbo Meya wa Manispaa ya Kigamboni amemshukuru Mhe.Rais na serikali yake Kwa jitihada za dhati za kuiletea maendeleo Tanzania kiuchumi, akirejea katika tukio la uwekaji jiwe la msingi 6/12/2021 katika kiwanda cha vifaa vya umeme cha Elsewedy cha Kisarawe II ambapo Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan aliweka jiwe la msingi na kuwaambia wanakigamboni kuwa kuna kitu kinaendelea kinachohusu uwekezaji Kwa hapa kigamboni hivyo wananchi watarajie uwekezaji mkubwa na kweli Leo hii tunashuhudia utiaji saini ili uwekezaji mkubwa wa aina yake kuanza ni furaha ilioje Kwa wanakigamboni ,yeye na Baraza la Madiwani wanaunga mkono juhudi zake .
Uwekezaji huu hadi kumalizika utagharimu Dola Bilioni 3,na Kwa awamu ya kwanza itatumika Dola milioni 400.Kwa awamu ya kwanza kutajengwa Viwanda 50 Hadi kukamilika vitakuwa Viwanda 100.Eneo ni la square mita za mraba mil.2.2 litakuwa na huduma za jamii ndani,Viwanda vya nguo,madawa na vya kuunganisha magari,barabara na taa zake,mtandao wa mawasiliano,matanki makubwa ya maji n.k.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa