Katika kuhakikisha Halmashauri nchini zinafikia azma ya Rais Samia Suluhu Hassani ya kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na anuani ya makazi ifikapo mei 2022, Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imefanikiwa kushika nasafi ya kwanza kimkoa kwa kufikia asilimia 102 za ukusanyaji wa taarifa za anuani za makazi.
Muwakilishi wa Mkurugenzi Charles Lawiso (Mwanasheria wa Manispaa) amebainisha hayo leo wakati alipokua akitoa mrejesho wa kazi nje ya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mjimwema na kuwapongeza wawezeshaji wa zoezi na vijana kwa ujumla kwa kufanya kazi kwa umoja na ufanisi na kuifanya kigamboni kushika nafasi ya kwanza mbali na changamoto zilizowahi jitokeza.
Mwanasheria amesema kuwa walilenga kuzifikia anuani 49,353 lakini wameweza kuzifikia anuani 50,545 na kuongeza kuwa, kijiografia Kigamboni inaeneo kubwa na mahali kwingine kufikika kwake imekua ni changamoto lakini wawezeshaji na vijana waliofanya kazi ya kukusanya taarifa wamefanikiwa kuyafikia.
"Nawaasa Vijana ikitokea kazi yoyote fanyeni kwa ufanisi, na sisi Manispaa tupo tayari kuwataumia katika matukio mengine ya kiserikali sababu tumeona ufanisi wenu" Alisema Mwanasheria
Kwa upande wake Muwezeshaji wa Manispaa Bi. Ariadina Peter amewapongeza vijana kwa kazi mbali na ugumu uliokuwepo lakini waliweza kuvumiliana na kubebana ili kuhakikisha lengo la Serikali linafikiwa.
Ameongeza kwa kusema kuwa zoezi hili limewasaidia vijana kujifunza mambo mengi ikiwemo jinsi ya kuongea na jamii lakini pia namna ya kufanya kazi kwa kuisoma jamii na hilo wamelifanya vizuri na ndio maana wamefanikiwa kuvuka asilimia.
Akizungumza kwa niaba ya wakusanya taarifa Selemani Anexwa amesema, wanashukuru kwa nafasi waliyopewa kwani walikua vijana wengi lakini Manispaa ikawaona wanastahili kupata ajira hiyo ya muda mfupi sababu waliwaamini.
"Asanteni kwa kutufikiria kwa mambo mengine kama Sensa na sisi tupo tayari kufanya kwa ufanisi zaidi sio kwasababu ya fedha lakini kwa uzalendo tupo tayari kutekeleza kazi zingine mtakazoona zinafaa na tunaomba radhi kwa mahali popote ambapo tulikiuka maadili" Alisema Selemani.
Selwmani ameongeza kusema kuwa wao kama vijana wamejifunza mambo mengi mbali na kufanyakazi lakini wameweza kufamimiana na kutengeneza (mtandao)connection baina yao.
Halmashuri ya Manispaa ya Kigamboni ina Tarafa 3, Kata 9 na mitaa 67 ambayo kwa kiasi kikubwa yote imefikiwa na taarifa zimekusanywa. Ikimbukwe zoezi la ukusanyi wa Tarifa za anuani za makazi lilianza rasmi tarahe 4/03 mara baada ya uzinduzi wa Kiwilaya.
Msoma ramani Bi. sada akiwafafanulia ramani ya eneo walilopo wakusanya taarifa za ananuani za makazi ili kuwawezesha vijana hao kutekelza jukumu lao.
Mandhari ya makazi ya Kigamboni.
Moja ya bango linaloonesha uelekeo wa barabara.
Muwakilishi wa Mkurugenzi Bw. Charles Lawiso (Mwanasheria wa Manispaa) akitoa mrejesho wa kazi leo kwenye eneo la ofisi ya Mtendaji Kata ya Mjimwema na vijana wa ajira ya muda waliokusanya taarifa za anuani za makazi.
Baadhi ya Vijana wa ajira ya muda waliokusanya taarifa za anuani za makazi wakisikiliza kwa makaini mrejesho wa kazi yao.
Vijana wakiwa kwenye moja ya mtaa kwa lengo la kuanisha nyumba na kukusanya taarifa za anuani za makazi
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa