Uongozi wa iliyokuwa Mamlaka ya Uendelezaji wa mji wa Kigamboni KDA(Kigamboni Development Agency) uliokuwa chini ya wizara ya radhi umekabidhi rasmi majukumu ya KDA kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni tarehe 17/4/2018 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali lililotolewa 13 septemba 2017 baada ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuvunja rasmi wakala wa uendelezaji wa mji Kigamboni.
Akikabidhi majukumu hayo aliyekuwa Mkurugenzi wa KDA (Kigamboni Development Agency) Bw.Dismas.W.Minja amesema kuwa ndani ya kipindi cha miezi sita walitakiwa kuwa wamekabidhi majukumu na wamefanya hivyo kwa muda uliopangwa.
Aidha amesema kuwa KDA uendeshwaji wake ulikuwa chini ya Wizara ya ardhi hivyo watakabidhi hati ya makabidhiano ya majukumu ya KDA pamoja na viambatanisho vyake.
Aliongeza kuwepo kwa ushirikiano baina ya Wizara ya Ardhi na Manispaa ya Kigamboni Katika kupanga, kupima na kumilikisha Ardhi ya Kigamboni kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibuzilizopo
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh. Maabad Hoja aliwashukuru uongozi wa KDA kwa kukabidhi majukumu hayo kwa muda uliopangwa na kuwaomba kuwapokea pindi watakapohitaji msaada zaidi kutoka kwao.
Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliopo Wizara ya Ardhi na kuhudhuliwa na wataalamu mbalimbali wa ardhi kutoka Manispaa ya Kigamboni .
Kaimu Katibu Mkuu wizara ya Ardhi Bi. Immaculata Senje wa kwanza Kushoto , akifuatiwa na Meya wa Manispa ya kigamboni Mh. Maabad Hoja na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Bi.Nice Mwakalinga wakisoma kwa makini Hati ya makabidhianoa ya majukumu ya KDA kabla ya makabidhiano.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni akisaini hati ya makabidhiano ya majukumu ya KDA kabla ya kukabidhiwa
Aliyekuwa Mkurugenzi wa KDA Bw.Dismas W.Minja akisoma kwa ufupi Hati ya makabidhiano ya majukumu ya KDA kabla ya kukabidhi kwa viongozi.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi.immaculata Senje kushoto akipokea Hati ya makabidhiano ya majukumu ya KDA kutoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa KDA Bw.Dismas Minja
Kaimu Mkurugenzi Bi.Nice Mwakalinga kushoto akipokea hati ya makabidhiano ya majukumu ya KDA kutoka kwa alyekuwa Mkurugenzi wa KDA
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh.Maabad Hoja kushoto akipokea hati ya makabidhiano ya majukumu ya KDA kutoka kwa aliyekuwa mkurugenzi wa KDA
Baadhi ya maandiko ambayo ni viambatanisho vinavyokabidhiwa kwa Manispaa ya Kigamboni
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mh. Maabad Hoja akitazama moja ya kiambatanisho kinachokabidhiwa na KDA
Baadhi ya viambata vilivyokabidhiwa na KDA
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa