Akizungumza wakati wa makabidhiano katibu tawala aliwataka wanafunzi kuwa na nidhamu na kuzingatia masomo kwa kuwa Serikali imefanya uwekezaji Mkubwa wa miundo mbinu katika sekta ya Elimu.
Naye Kaimu Mkurugenzi bi Sigilinda Mdemu ambaye ni Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii ameipongeza na kushukuru TASAF kwa kuona umuhimu wa kutoa vifaa vya usafi kwa mabinti wa shule ya lingato kwani wamesaidia kupunguza gharama kwa wazazi wa wananfunzi hao.
"Nakupongeza mratibu wa TASAF (w) sambamba na Afisa ufuatiliaji kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa hivi ambavyo ni msaada mkubwa kwa watoto wetu". Alisema Sigilinda.
Aidha Mwenyekiti wa Mtaa wa Lingato Mh Cosmas Sombi ametoa pongezi kwa viongozi wa Wilaya na Halmashauri kwa kuendelea kusimamia vyema ujenzi wa miundo mbinu ya elimu na malezi kwa watoto wanaosoma shule zote zilizopo wilayani humo ikiwemo shule ya Lingato.
Sambamba na hilo Mhe. Sombi amesisitiza wazazi kusimamia elimu za watoto wao kwa kuhakikisha wanafika shule na kushirikiana na walimu katika kuwezesha upatikanaji wa elimu bora huku wakihakikisha watoto wanapata chakula shuleni ili kuongeza ufaulu.
Mhe sombi amekua miongoni mwa viongozi wa mfano katika wilaya ya Kigamboni kwa kuwa anasimamia vyema upatikanaji wa chakula shuleni na kwa shule ya sekondari ya Lingato ameendelea kutoa mahitaji ya chakula kwa wanafunzi 129 wanaosoma shuleni hapo.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa