Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafairi kupitia katibu tawala wa Wilaya Dalmia Mkiaya leo ametimiza ahadi ya kutoa mifuko ya sementi 197 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa kabla ya kuhamishwa kituo cha kazi pindi alipokuwa akifanya ziara ya kikazi ya kutembelea Shule za Msingi na Sekondari ili kutazama miundombinu yake na kuona namna kuimarisha.
Katibu Tawala wa Wilaya Dalmia Mikaya amesema kuwa wanatamani sekta ya Elimu Kigamboni ipige hatua na ndiomaana ilimpendeza Mkuu wa Wilaya kuhakikisha anatafta namna ya kupata sementi zitakazowezesha kuboresha miundombinu ya shule kwa kufanya ukarabati wa maeneo mbalimbali kulingana na uhitaji wa shule husika.
Aidha amewataka walimu wa shule za Msingi na Sekondari waliofika kuchukua sementi hizo kuzitumia kulingana na mahitaji waliyoombea na kuhakikisha pia wanasimamia vyema miundombinu ya Shule ikiwa ni pamoja na kusimamia vyema fedha wanazopokea kwa miradi ya maendeleo katika Shule zao.
Jumla ya mifuko 197 imekabidhiwa ambapo Shule za msingi imepata jumla ya mifuko 137 na ukabidhiwa kwa shule 7 ambapo kila shule imepata mifuko 20 isipokuwa shule moja iliyopata mifuko 17, Mifuko 60 imekabidhiwa kwa shule 3 za sekondari ambapo kila shule imepata mifuko 20.
Katibu tawala amesema kuwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya bado itaendelea na jitihada za kuchangia maendeleo ya Elimu na maeneo mengine kwa kadri watakavyokuwa wanapokea misaada kutoka kwa wadau mbalimbali.
Baadhi ya mifuko ya Sementi iliyokabidhiwa.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa