KAPU LA MAMA KIGAMBONI WANUFAIKA MADARASA 10 YAJENGWA
Katika kuboresha miundombinu ya elimu ya sekondari na kutatua changamoto za kukaa wanafunzi madarasani serikali imeendelea kutatua changamoto hizo kwa kuelekeza fedha katika sekta ya Elimu ili kuboresha mazingira ya ufundishaji na kujifunza.
Manispaa ya Kigamboni ni moja ya Manispaa zilizonufaika na uboreswaji WA sekta ya Elimu ambapo katika mengi pia imepokea kiasi cha shilingi milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 10 yatakayotumika kwa wanafunzi wa kidato cha Kwanza kwa mwaka 2023.
Katika utekelezaji huo Manispaa imefanikisha kujenga vyumba hivyo kwa ustadi wa hali ya juu ambapo madarasa ni ya kisasa kabisa yenye vioo,feni na sakafu yenye marumaru.
Katika utekelezaji huo shule ya sekondari Kisota umepata darasa 1,Aboud jumbe darasa 1,Pembamnazi darasa 1, Kisarawe II darasa 1,Kibada darasa 1,Kidete darasa 1,Kimbiji darasa 1, Minazini darasa 1 na Mizimbini darasa 1.
Hongera serikali kwa kutekeleza Ilani ya CCM.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa