*KAMPUNI YA ORYX ENERGIES YATOA MITUNGI 5 NA MAJIKO 5 KWA SHULE 5 (MSINGI NA SEKONDARI) KATA YA VIJIBWENI*
Leo Mei 09, 2023 Kampuni ya Oryx Energies imetoa Jumla ya Mitungi 5 ya gesi na Majiko 5 kwa Shule 5 (2 za Sekondari na 3 za Msingi ) zilizopo ndani ya Kata ya Vijibweni Wilayani Kigamboni.
Hafla hiyo fupi ya kukabidhi mitungi hiyo kwa Walimu Wakuu wa Shule husika, imefanyika katika viwanja vya nje vya Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Vijibweni ambapo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Zacharia Mkundi maarufu kwa jina la White.
Katika maelezo yake, Meneja wa Kampuni ya Oryx Energies kanda ya Pwani Bw. Shabani M. Fundi amesema kuwa lengo la wao kufanya hivyo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha ile sera ya uwepo wa chakula mashuleni kwa Wanafunzi inatekelezwa ipasavyo haswa kwa kutumia nishati ya gesi katika kupika ikiwa ni kuondokana na changamoto ya kutumia kuni au mkaa.
Naye Mratibu wa Elimu kata ya Vijibweni alisema "Tunashukuru sana , tulikaaa tukaona gharama za upatiakanaji wa chakula shuleni ni mkubwa sababu tulikuwa tunatumia kuni na mkaa, tuliandika barua oryx na leo wamejibu kwa vitendo, tunashkuru sana na tuwahakikishie hizi gesi na majiko yatakwenda kutumika vema na tutashirikiana nanyi wakati wote."
#KaziIendelee
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa