KAMATI YA USHAURI WILAYA YA KIGAMBONI YAPITIA RASIMU YA BAJETI 2023/2024 NA KUIDHINISHA TSHS BIL.57.4
Leo tarehe 16/2/2023 Kamati ya ushauri ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh.Halima Bulembo imekaa kikao chenye lengo la Kupitia Rasimu ya Bajeti ya 2023/2024 .
Akiongea katika kikao hicho mara baada ya kujitambulisha amewapongeza wote kwa namna moja ama nyingine waliofanikisha kutekeleza kwa miradi ya maendeleo akiwepo Mkurugenzi na watumishi wote wa Manispaa katika utekelezaji wa miradi .
Akizungumzia lengo la kikao amesema lengo ni kupokea na kujadili mapendekezo ya Rasimu ya Bajeti ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Manispaa amesema anategemea maoni yao katika kupitia Rasimu hii ambayo yatakuwa yenye kujenga Kwa ajili ya maendeleo ya Manispaa.
Aidha amemtaka meneja wa TARURA kufanya ushawishi ili kuongeza Bajeti ya barabara angalau kufikia lengo,pamoja na Hilo amewataka wananchi kuacha kukopa mikopo ya Kaushal damu kwani si sahihi hivyo amewataka viongozi ngazi zote kuwaelimisha wananchi kutojiiingiza katika mikopo hiyo kwani inawaingiza katika matatizo na haiwasaidii kujikwambua kwa kuanzisha biashara hivyo amewataka kujikita katika mikopo ya Halmashauri ambayo haina riba kabisa.
Akiwapitisha wajumbe katika Rasimu hiyo Mchumi wa Manispaa ya Kigamboni bi.Flora Nyanana amesema Bajeti hiyo imezingatia muongozo elekezi na ikilinganishwa na ya mwaka Jana imeongezeka kwa asilimia 25.Akitaja moja ya mikakati wa kuongeza mapato amesema itajengwa hostel ya kisasa ya ghorofa kwa ajili ya kuwapunguzia adha wanafunzi.
Akiongea Mbunge wa Kigamboni amesema kwa upande wa suala la Michezo kuna Juhudi nyingi zimefanyika kuhamasisha Wadau kuja kuendeleza Michezo moja wapo ni Machava ambapo kuna kiwanja kizuri cha mpira wa kikapu kwa msaada wa Wadau .Kwa upande wa barabara amesema barabara itajengwa kiwango cha lami kupitia mradi wa DMDP kilomita 100 za barabara katika Kata zitajengwa katika kiwango cha lami kufikia mwishoni mwa mwaka utekelezaji huo utakuwa unaanza,lakini pia katika kutatua tatizo la kuchonga barabara Manispaa imejipanga katika Bajeti hii itanunua greda ambalo litatatua kero ya uchongaji wa barabara.Aidha Bajeti hii itaenda kuongeza na kuboresha huduma za mama na mtoto.
Akiongea Meya wa Manispaa Mh.Ernest Mafimbo amegusia suala la mikopo kuchukua muda tofauti na mikopo ya mitaani amefafanua kuwa mikopo hii hutolewa kwa kila Robo hivyo ndani ya mwaka hutolewa mara nne na hufuata utaratibu maalum hadi kumfikia mkopaji.
Wakitoa maoni mbalimbali wajumbe hao wameongeza utekelezaji wa miradi ya Elimu na afya katika Manispaa ya Kigamboni,lakini pia wametaka Bajeti kujikita pia katika maswala ya Michezo kwani Michezo ni ajira ,miundo mbinu ikiwepo barabara kuhakikisha zinajengwa kwa kiwango cha lami hivyo pesa ziwekwe kwa kuzingatia hilo ikiwepo mitaro ili kudhibiti suala la mafuriko aidha katika Bajeti upande wa maendeleo ya jamii wametaka Bajeti ijikite katika kutekeleza shughuli za kudhibiti maadilibkwani maadili katika jamii yameshuka .
Nae Mkurugenzi ndg.Erasto Kiwale akifafanua baadhi ya maoni yaliyotolewa na wajumbe katika suala la Michezo na Machinjio amesema kuna yaliyofanyiwa kazi tayari mfano suala la machinjio ilishaanza kujengwa katika Kata ya Somangila na ujenzi upo katika hatua ya upauaji na ujenzi unaendelea,na kuhusu Michezo amesema Juhudi zimefanyika katika ufukwe wa umma wa Kidete imetengwa sehemu ya uwanja na kuwekwa magoli na tayari unatumika kwa mpira wa miguu.
Akifunga kikao hicho DC Bulembo amewashukuru wajumbe na kuwaomba ushirikiano wa dhati ili kuendeleza Kigamboni na kufikia malengo kwa urahisi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini KGMC
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa