Tarehe 28/07/2022 Kamati ya ulinzi na usalama wa mwanamke na mtoto ngazi ya Wilaya ilikaa kikao na kujadili jinsi ya kutokomeza vitendo vya ukatili.Wajumbe wa Kamati hiyo waliazimia kwa kuweka mikakati 5 ambayo itatekelezwa kwa lengo la kupaza sauti kwenye Jamii kwa kupiga vita vitendo vya ukatili vinavyo ongezeka kwa kasi kubwa kwenye jamii zetu.
Bi.Sereti L.Kiroya Afisa Ustawi Kiongozi Manispaa ya Kigamboni alitoa pongezi za dhati kwa Maafisa Ustawi wa Jamii na wajumbe wa Kamati za ulinzi na usalama wa mwanamke na mtoto ngazi ya Kata 4 ambazo walikaa vikao vyao kota ya mwisho wa mwaka na kujadili namna ya kupaza sauti kwenye jamii kwa kupinga vitendo vya ukatili kwa watoto,wanawake na wanaume.
Kamati hizo ziliweza pia kuandaa mpango kazi wao wakuwawezesha kufikia lengo walilokusudia kwenye jamii.Kamati hizo ni Kata ya Vijibweni,Mji Mwema,Kibada na KisaraweII.
Aidha Bi.Sereti ametoa ombi na ukumbusho kwa mabaraza mengine ya Kata na Mitaa ya ulinzi na usalama wa mwanamke na mtoto kuwa na muamko wa kufanya vikao kila kota ya mwaka ili kutokomeza vitendo vya ukatili kwenye jamii.
"TUKATAE UKATILI,SISI SOTE NI MASHUJAA"
IMETILEEW NA KITENGO CHA MAWASULIANO SERIKALINI
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa