Leo Agost 14. 2024 kamati ya siasa ya Wilaya ya Kigamboni ikiongozwa na mwenyekiti wake CDE. Sikunjema Shabani imefanya ziara ya kutembelea na kukagua Miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Manispaa ya Kigamboni.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo CDE Sikunjema amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha kwaajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo katika sekta ya Afya, Elimu pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya barabara.
"Kigamboni imebadilika sana, Kigamboni inazidi kupata miradi ya maendeleo. Alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha katika ziara hiyo aliutaka uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kuwapa kipaumbele na kuwatumia mafundi ujenzi walipo katika Manispaa hiyo wakati wa ujenzi miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuwapa fursa ya kupata ajira itakayowasaidia kujipatia kipato.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa shule mpya ya Sekondari ya Vumilia ukooni Diwani wa Kata ya Kisarawe ii Mhe. Issa Zahoro ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuleta fedha kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo ambayo itawasaidia kuwapunguzia wanafunzi umbali kwa kutembea kilomita 12 kwa kufuata huduma ya Elimu.
Katika ziara hiyo kamati ilifakiwa kutembelea na kukagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Vumilia ukooni, kata ya Kisarawe ii, Kituo cha Afya cha Mjimwema, kata ya Mjimwema, ujenzi wa jengo la huduma ya Mama na Mtoto, Kata ya Vijibweni, ujenzi wa barabara ya Chagan polisi, Kata ya Kigamboni pamoja na ujenzi wa karavati Kata ya Somangila,
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa