Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sara Msafiri leo amefungua rasmi kamati ya Maafa ya Wilaya yenye lengo la kufuatilia matukio yote ya majanga na kuhakikisha usalama wa wananchi na kumtaka Mkurugenzi waManispaa kuhakikisha kunakuwepo na CMT( vikao vya menejiment) maalumu maramoja kwa mwezi vya kupokea taarifa kutoka kwenye kamati zilizopo ngazi ya Kata ili zisaidie katika utekelezaji.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo kwenye ukumbi wa mikutano uliopo ofifi za Mkurugenzi Mhe. Sara amesema kuwa Kamati kama hii ni muhimu kwa majanga makubwa na hata madogo kama madhara yatokanayo na mvua ambayo yanaathiri wananchi kwa kiwango kikubwa hususani kwa Kigamboni ambayo bado inachangamoto ya miundombinu.
Mhe Sara ameongeza kwa kusema ni kweli kunachangamoto sana kuhusu maafa lakini haiwezekani kuacha yaende kama yalivyo au kutegemea kiongozi mmoja asimamie kwakuzingatia maendeleo yanaenda sambamba na uharibifu hivyo suala la maafa ni lazima kuwekea mikakati ya kudhibiti na pale inapotokea ifahamike yatakabiliwa vipi.
Aidha Mkuu wa Wilaya amessiitiza ushirikiano baina ya wajumbe wote wa kamati hiyo hususani kutoka katika taasisi mbalimbali kwa kuwa uwezo na nguvu wanayo kuhakikisha malengo yaliyopangwa yanatekelezeka kwa muda sahihi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Bi.Catherine Mashalla amepokea maagizo na kusema kuwa Maafa yapo na yataendela kuwepo lakini jambo pekee ni muhimu kukabiliana nayo kwa kutengenezea mikakati itakayosaidia kupunguza changamoto katika wilaya yetu hivyo wajumbe wote waliochaguliwa kuunda kamati wamejiandae kuwajibika vyema pindi majumu rasmi yatakapoanza.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa