Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imezindua rasmi Kamati ya Lishe yenye lengo la kukabiliana tatizo la upungufu wa madini joto ambapo kwa Tanzania limeathiri kwa kiwango kikubwa.Madini joto ni muhimu kwa mwili wa binadamu hususani kwenye siku 1000 za maisha yake yote ( tangu mtoto akiwa tumboni kwa mama yake na hadi kufikia miaka miwili ya ukuaji wake).
madini joto husaidia ukuaji wa akili ya mtoto na kumsaidia kuepukana na udumavu wa akili, husaidia kutengeneza tezi za shingo, mfumo wa fahamu, mwili na ubongo na ukuaji wa mwanadamu kwa ujumla. kamati hii ya lishe imelenga kuhakikisha jamii nzima ya kigamboni inaeleimishwa na kueleweshwa umuhimu na namna ya upataikanaji wa madini joto tangu mtoto akiwa tumboni kwa mama yake hadi kipindi cha miaka miwili cha ukuaji wake.
upungufu wa madini joto ukikosekana mwili hupelekea athari za kudumaa kwa akili,mtoto kuzaliwa na mtindio wa ubongo,kuwa kiziwi/bubu, kuchelewa kwa balehe kwa watoto wanaokaribia balehe na mtoto kuchelewa kwenye hatua za ukuaji na hatimaye kudumaa kabisa na kuvimba kwa tezi.
Kamati hii ya Lishe ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji inalenga kusaidia jamii kuondokana na madhira yanayoweza kusababisha kwa kukosekana kwa madini joto ili kuwa na vizazi bora na vyenye uelewa mzuri katika kuendeleza nchi yetu.Kamati hii itashirikisha wajumbe kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Kata, viongozi wa madhehebu na mashirika yasiyo ya serikali.
Kikao cha uzinduzi wa kamati ya lishe ya Wilaya kimefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano uliopo Kata ya Mjimwema ambapo wajumbe mbalimbali walihudhuria wakiongozwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa