Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa ambapo kilishirikisha wajumbe kutoka katika idara na vitengo Mtambuka vinavyounda kamati hiyo ambazo ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Maendeleo ya Jamii, Elimu Msingi na Sekondari usatwi wa jamii, Mipango uratibu na ufuatiliaji, Huduma za sheria pamoja na fedha na uhasibu
Akiiwasilisha bajet hiyo Afisa Lishe wa Manispaa ya Kigamboni Bi. Henerietha Henry amesema lengo la kikao hicho ni kujadili shughuli mbalimbali za lishe zitakazoingizwa kwenye Mpango na bajeti ya lishe ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwa kuzingatia changamoto zilizojitokeza kwa Mwaka wa fedha ulioisha ikiwemo; tatizo la upungufu wa damu kwa Mama wajawazito, lishe kwa vijana balehe, utoaji wa chakula Mashuleni, uzito uliozidi na viribatumbo, watoto kuzaliwa na uzito pungufu wa chini ya kg 2.5 n.k
Hata hivyo Afisa lishe wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi Mwanamvua Zuberi pamoja na Mganga Mkuu wa Manispaa Dkt. Lucas Ngamtwa wameishauri kamati hiyo kuongeza makadirio ya bajeti ya mwaka kwa watoto kutoka 1000 hadi 1500.
Aidha Bi Mwanamvua pia amewashauri wataalam wa Kamati hiyo kuandaa bajeti ambayo ni shirikishi kwa sekta zote ili iwe rahisi kurejea wakati wa utekelezaji
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa