Kamati ya kudhibiti UKIMWI Manispaa ya Kigamboni ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Stephano Warioba leo imepewa mafunzo yenye lengo la kujengea uwezo kamati shirikishi kwa ngazi ya Manispaa kuweza kuratibu na klusimamia jitihada za kupambana na VVU na UKIMWI ili kufikia male ngo ya Manispaa, Mkoa, Taifa na Kimataifa.
Mafunzo hayo yametolewa na Yahaya Mmbaga Mratibu wa Dawati la Mikoa na Halmashauri TACAIDS na kusema mafunzo haya yanalenga kutoa tathmini ya VVU na UKIMWI katika Manispaa na kuweka mikakati ya Kila Mwaka, kuunganisha wadau wanaotekeleza afua za UKIMWI na kutathamini uwajibikaji wao,kuhakikisha utekelezaji wa sera , Mikakati ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI, sheria miongozo na matokeo ya tafiti mbalimbali yanafanyika, kuratibu, kufuatilia kutathmini utekelezaji wa shughuli za vvu na UKIMWI zilizopangwa.
Ameongeza kwa kusema kuwa Taifa limeendeleakushuhudia kupungua kwa maambukizi mapya ya VVU ikilinganishwa na miaka ya 1990 kutoka asilimia 7 mwaka 2013 hadi asilimia 4.7 mwaka 2016 ambapo amesemakupungua kwa maambukizi ya VVU ni matokeo ya juhudi mbalimbali za Serikali na wadau ikiwemo Taasisi za dini ingawa madhara kwa jamii na Taifa kwa ujumla bado ni makubwa.
Akizungumzia hali ya maambukizi kwa Kigamboni Dkt.David Manyama ambaye Mratibu wa Maambukizi wa Virusi vya Ukimwi ni amesema kuwa Januari 2018 maambukizi yalikuwa asilimia 2, mwaka 2019 maambukizi yalikuwa asilimia 6 na kwa mwaka 2020 hali ya maambukizi ilishuka hadi kufikia asilimia 4.
Yahaya Mmbaga Mratibu wa Dawati la Mikoa na Halmashauri TACAIDS akitoa mafunzo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo.
Yahaya Mmbaga Mratibu wa Dawati la Mikoa na Halmashauri TACAIDS akitoa mafunzo.
washiriki wamafunzo wakifatilia kwa makini.
Dkt.David Manyama ambaye Mratibu wa Maambukizi wa Virusi vya Ukimwi akielezea hali ya maambukizi Kigamboni.
Gezaulole Kata ya Somangila, Kigamboni
Anuani ya Posta: 36009 Dar es Salaam
Simu: +255222928468
Simu ya Mkononi: +255222928468
Bara pepe: info@kigambonimc.go.tz
Haki MilikiĀ©2017 Manispaa ya Kigamboni . Haki zote Zimehifadhiwa